Jedwali hili hapa chini ni summary tu ya matokeo hayo kwa 
ujumla.
 Baraza la mitihani la Taifa, NECTA, limetangaza matokeo ya mtihani wa 
kidato cha nne uliofanyika mwezi November mwaka jana, huku kiwango cha 
ufaulu wa masomo ukipanda kati ya asilimia 0.16 na 16.72 ikilinganishwa 
na mwaka 2012, na wasichana wakiibuka kidedea katika ufaulu wa jumla 
kitaifa. 
Jumla ya watahiniwa 
235,227 sawa na asilimia 58.25 ya watahiniwa wote wamefaulu mtihani, 
idadi ya wasichana ikiwa 106,792 na wavulana 128,435, tofauti na mwaka 
2012 ambapo waliofaulu walikuwa ni 185,940. 
Kaimu katibu 
mtendaji wa NECTA, Dkt. Charles Msonde anatangaza rasmi matokeo haya, 
ambayo yanaonyesa ufaulu kimasomo ukiongozwa na somo la Kiswahili, kwa 
asilimia 67.77 huku somo la hisabati likiendeleza historia ya kushika 
mkia, kwa ufaulu wa asilimia 17.78.
Kati ya watahiniwa kumi 
bora waliofanya vema kitaifa, saba kati yao ni wasichana wakitokea shule
 za Marian girls, St. Francis Girls na Cannossa. 
Lakini ni 
viwango vipi vimetumika katika usahihishaji wa mtihani huu, kwa 
kuzingatia mkanganyiko uliojitokeza kuhusiana na madaraja ya ufaulu?
Aidha, NECTA imefuta matokeo yote ya mtihani kwa watahiniwa 10 
waliobainika kuandika matusi katika karatasi zao za majibu, na adhabu 
hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 6(2)(a) cha kanuni za mtihani.
Aidha baraza hilo limefuta matokeo yote ya mtihani kwa watahiniwa 272, 
waliobainika kufanya udanganyifu kwa njia mbalimbali, ambapo watahiniwa 
242 ni wa shule, 19 ni watahiniwa wa kujitegemea na 11 ni wale wa 
maarifa ama QT.
Shule zilizojitokeza kufanya vizuri zaidi ni 
Marian wasichana na wavulana, St. Francis wasichana, Anne Maria, 
Kizirege, Cannossa na shule ya mwisho kwa kigezo cha watahiniwa zaidi ya
 40 ikiwa ni Kitonga na chini ya watahiniwa 40 ikiwa ni shule ya 
Uchindile ya Morogoro.
Mwisho.
Hizi ndio shule 10 bora matokeo kidato cha nne 2013:
1. St.Francis Girls (Mbeya)
2. Marian Boys (Pwani)
3. Feza Girls (Dar-es-salaam)
4. Precious Blood (Arusha)
5. Canossa (Dar-es-salaam)
6. Marian Girls (Pwani)
7. Anwarite Girls (Kilimanjaro)
8. Abbey (Mtwara)
9. Rosmini (Tanga)
10. DonBosco Seminary (Iringa)
Hawa ndio wanafunzi 10 bora matokeo kidato cha nne 2013:
1. Robina S Nicholaus (Marian Girls - Pwani)
2. Magreth Kakoko (St. Francis Girls - Mbeya)
3. Joyceline Leonard Marealle (Canossa - Dar-es-salaam)
4. Sarafina W. Mariki (Marian Girls - Pwani)
5. Abby T Sembuche (Marian Girls - Pwani)
6. Sunday Mrutu (Anne Marie - Dar-es-salaam))
7. Nelson Rugola Anthony (Kaizirege - Kagera)
8. Emmanuel Mihuba Gregory (Kaizirege - Kagera)
9. Janeth Urassa (Marian Girls - Pwani)
10. Angel Ngulumbi (St. Francis Girls - Mbeya)
Matokeo yanapatikana  kupitia tovuti zifuatazo:
Pia, matokeo yanaweza kupatikana kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kupitia namba 15311. Jinsi ya kutuma ujumbe, Andika: MatokeoXNamba ya kituoXNamba ya Mtahiniwa
Mfano: matokeoxS0101x0503

No comments:
Post a Comment