Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Thursday, July 3, 2014

HAYA NDIYO MAJIBU YA ADAM MCHOVU, B12 NA DJ FETTY BAADA YA SAKATA YA KURUSHIANA MAKONDE NDANI YA STUDIO ZA CLOUDS HAPO JANA


Kama ulikuwa Hewani siku ya jana katika kipindi maarufu kabisa (XXL), ndani ya Stetion maarufu hapa Tz yaana nazungumzia CLOUDS Fm utaelewa nini ninachozungumzia mpaka sasa. Katika hali isiyotegemewa jana watangazaji watatu maarufu kama, DJ FETTY, ADAM MCHOVU na B12 waliziweka ndani ya studio za Clouds live huku wakisahau kuwa Wasikilizaji wanawasikia mwanzo mwisho wanachokifanya huko ndani ya studio. Sakata hilo limesababisha na kutoelewana baina ya hawa watangazaji juu ya mauzo ya Albam ya Fiesta! kama hukupata Fursa ya Kusikiliza 

Sasa leo watu mbalimbali na wasikilizaji walikuwa nataka kujua nini zaidi kilitokea kupitia kipindi cha Hekaheka, chanzo cha ugomvi hasa ni nn?
Baada ya massage nyingi sana kwenye kipindi cha hekaheka ilibidi wahusika wanyanyue simu zao kuwatafuta Adam, Fetty na B12 kujua nini kilichosababisha kuchapana makonde wakati bado kipindi kikiwa hewani. Muhusika alinyanyua moja kwamoja simu na kumpigia B12 ambaye alikataa kabisa kueleza chanzo cha sakata hilo la kutwangana huku akisema mambo yote yapo kwa uongozi.....
PICHA YA STUDIO ZA CLOUDS BAADA YA KUZICHAPA
Simu ya pili ilimuendea ADAM MCHOMVU ambaye pia aligoma kuelezea kilichotokea jana, baada ya Muda mfupi Adam alimkabidhi Dem wake ili azungumze na mwandishi, huku akijua kwamba harikodiwi kumbe yupo hewani, alikiambia kipindi cha hekaheka kwamba ADAM amemaind na hataki kuongea na simu!! 

Simu ya tatu ilienda kwa DJ FETTY, Ambapo iliita bila majibu kwamba ilikuwa haipatikani..
Chanzo kinasema kwamba baada ya ugomvi, vifaa mbalimbali vya studio vimeharibiwa wakati wa ugomvi huo kama MIC, COMPUTER Meza nk.  Endelea Kufuatilia Hapa ili ujua ni hatua Gani watachukuliwa watangazaji hawa kwa kukosa utovu wa Nidhamu

No comments:

Post a Comment