Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Saturday, January 10, 2015

NEWS:AJALI YA MBUNGE WA MBEYA MJINI MH;JOSEPH MBILINYI ILIYO TOKEA MLIMA KITONGA LEO

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu' amenusu kifo baada ya gari aliyokuwa akisafiria kupata ajali katika eneo la mlima Kitonga mkoani Iringa. Taarifa za awali kutoka kwa katibu wake Kwame Anangisye zimeeleza kuwa Mbunge huyo akiwa na watu wanne kwenye gari yake alipata ajali hiyo mwanzoni mwa mlima Kitonga akitokea Mbeya kuelekea jijini Dar es Salaam.
“Tulipoanza kushuka kwenye mlima Kitonga gari ya Mbunge ilifeli breki na kisha kupinduka mara moja na kugeukia ilikotokea, ilikuwa ajali mbaya lakini tunashukuru Mungu  tumepona.
Amesema pamoja na ajali hiyo kuonekana  mbaya kwao,  wanamshukuru Mungu kwani waliweza kutoka wakiwa salama na hakuna hata mmoja aliyepata maumivu makali.
Kwa habari Zaidi ungana nasi baadaye.

No comments:

Post a Comment