Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Tuesday, October 22, 2013

BODI YA UTALII TANZANIA YASHAURI IRINGA IJIPANGE


Bw. Geofrey Meena- Meneja masoko wa bodi ya Utalii nchini, akipata dondoo za kuboresha sekta ya utalii, katika kikao kilichowashirikisha wadau wa sekta hiyo mkoani Iringa, kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Hotel ya MR.
Bw. Sam Kasulwa- Ofisa Uhusiano wa bodi ya Utalii nchini, akitoa ushauri katika kikao hicho kilichowashirikisha wadau wa Utalii mkoani Iringa. 
  Wadau wa utalii wakisikiliza ushauri unaotolewa na viongozi wa bodi. 
Bw. Ernest Lugala (mwenye Tshirt nyekundu) akiwa na wadau wenzie katika kikao hicho. 
 Bw. Zabron Luvinga mdau wa sekta ya Utalii, na mmiliki wa Hotel ya MR akiandika machache yahusuyo uboreshaji wa sekta ya utalii mkoani Iringa.


 Bw. Lugangira mmoja kati ya wadau wa utalii, akiwa katika kikao hicho, katika hotel ya MR  mjini Iringa
Bw. Ernest Lugala akichangia mawazo juu ya kuboresha sekta hiyo nchini. 
 Mdau akichangia mada juu ya nini kifanyike katika kuinua sekta ya utalii mkoani Iringa.
 Bw. Alban Lutambi kutoka Hotel ya Ruaha Hilltop, kati ya Hotel za kitalii mkoani Iringa akitoa mawazo yake katika kikao hicho.
 Bw. Zabron Luvinga mmiliki wa Hotel ya MR  iliyopo mjini Iringa, moja ya Hotel za kitalii mkoani humo.

Afisa utamaduni wa Manispaa ya Iringa Bw. Kadinde akisikiliza kwa umakini ushauri kutoka kwa viongozi wa bodi ya Utalii, hiyo ikiwa ni sekta yake katika idara ya Utalii.

MKOA wa Iringa umetakiwa kujipanga vyema kwa kujenga miundombinu bora ya utalii ili kulinda hadhi ya kuwa kitovu cha Utalii kwa kanda ya mikoa ya Kusini.

Ushauri huo umetolewa na ofisa mahusiano wa bodi ya Utalii nchini Bw. Sam Kasulwa wakati wa kikao cha wadau wa bodi ya Utalii, kilichofanyika katika ukumbi wa Hotel ya MR mjini Iringa.
Kasulwa amesema kuna haja kwa wadau wa utalii kujenga Hotel za kisasa zenye hadhi ya nyota tano na sita ili kuweza kumudu kuwapokea watalii na wageni wa kitaifa na kimataifa.

"Kila kikao tunaulizwa swali hili hili la kuwa kwa nini mikoa ya kusini haijapewa kipaumbele cha kutangazwa licha ya kuwa na utajiri wa vivutio, ukweli ni kuwa mikoa ya kaskazini ilianza muda mrefu kujitangaza, na ndiko kukajengwa miundombinu bora ya utalii, sasa na nyinyi Iringa ili mtangaze vivutio vya utalii mlivyonavyo mnapaswa kujiandaa kwa miundombinu bora naya kisasa, hasa barabara, usafiri wa anga na kujenga hotel zenye hadhi ya kupokea watalii," Alisema Kasulwa.

Naye meneja masoko wa bodi hiyo ya Utalii Bw. Geofrey Meena amesema kutokuwepo kwa huduma bora, kuanzia mapokezi hadi katika hotel za kuwalaza wageni ni moja ya sababu inayochangia wageni wengi kukimbia na hivyo kutangaza sifa mbaya kwa wenzao juu ya utalii nchini.

Meena amesema kuna haja ya watanzania wenyewe kuwa mabarozi wazuri wa kuutangaza utalii kwa wageni, kwa kutumia mazungumzo mema yenye kuitangaza vyema nchi katika sekta ya utalii.

"Sisi wenyewe hapa tunapaswa kuwa mabarozi wazuri wa utalii, tuzungumze lunga nzuri tunapokuwa na wageni kwa kuisifia nchi yetu na utalii uliopo, utalii uwe ni kipaumbele chetu kikuu,  kwa kuboresha hotel zetu," Alisema Meena.

Afisa masoko na mkuu wa bodi ya utalii Peter Mkumbo amesema katika miundombinu inayolegalega na kudhorotesha sekta ya utalii ni pamoja na usafiri wa anga wa ndani na nje ya nchi, hali inayochangia mapato makubwa ya utalii kupotea.


Hata hivyo Albano Lutambi kutoka Ruaha Hilltop amesema changamoto nyingine ni pamoja na mabarozi wa utalii kutokuwa na ufahamu mzuri juu ya kile wanachotakiwa kukitangaza kama ndiyo kazi yao.
"Changamoto kubwa jamani hata hawa mabarozi wa utalii baadhi yao hawafahamu kabisa nini wanatakiwa kufanya katika idara yao, kwanza unakuta hata upande wa lugha siyo mzuri sana, kwa maana ya kuwa anakuwa anauwezo wa kuzungumza lugha moja tu, ipo haja ya kuwapa elimu zaidi watambue wajibu wao, lakini pia wajue hata zaidi ya lugha mbili," Alisema Lutambi.

No comments:

Post a Comment