Mbunge Amina Mwidau, akihutubia wanannchi wa Wilaya ya Pangani katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo Mkoa wa Tanga.
Mbunge
Mwidau akiwa na Ofisa Utamaduni na Michezo wa Wilaya ya Pangani, Kemmy
Anatory mara baada ya kuzindua mashindano ya Mwidau

CUP.


……………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu, Tanga
MBUNGE
wa Viti maalum Mkoa wa Tanga Amina Mwidau (CUF), amewataka wananchi wa
Mkoa wa Tanga kubadilika kwa kuwa na ari ya kujiletea maendeleo yao na
jamii kwa ujumla.
Kauli
hiyo ameitoa mjini hapa alipokuwa akizungumza na vionozi wa Chama cha
Waandishi wa Habari Mkoa wa Tanga (Tanga Press Club).
Alisema kuwa ili maendeleo ya haraka yaweze kupatikana katika mkoa huo ni lazima jamii kubadili kwa kuwa na mawazo chanya.
“Maendeleo
ni jambo muhimu sana na katika hili ni lazima tushirikiane kwa dhati.
Binafsi ninapenda kupongeza juhudi za chama cha Waandishi wa habari Mkoa
wa Tanga kwa kazi kubwa na nzuri wanayofanya katika kutangaza mkoa
wetu.
“Nilikuwa
nasoma na sasa kila wakati tutakuwa pamoja na wanahabari pamoja na
wananchi wa mkoa wetu ili kuweza kuungana kwa pamoja katika juhudi za
maendeleo za mkoa,” alisema Mwidau
chanzo fullshangwe.
No comments:
Post a Comment