Mwenyekiti wa Pembejeo za Kilimo Wilaya ya Njombe Bi. Sarah Dumba Akielezea Juu ya Zoezi la Usambazaji wa Pembejeo za Ruzuku za Kilimo.
Serikali Wilayani Njombe Imeanza Zoezi la Kusambaza Pembejeo za Kilimo za Ruzuku Kwa Wakulima wa Wilaya Hiyo Kwa Ajili ya Kuanza Maandalizi ya Kilimo Huku Ikitoa Angalizo Kwa Watumishi Wenye Tabia ya Kujiandikisha Kwa Ajili ya Kupatiwa Pembejeo Hizo.
Akiongea na mwandishi wetu Mwenyekiti wa Kamati ya Pembejeo Wilaya ya Njombe Bi. Sara Dumba Ambaye Pia ni Mkuu wa Wilaya Hiyo Amesema Jumla ya V0cha Elfu Tisa Zitasambazwa Kwa Watu Wenye Sifa za Kupata Pembejeo Hizo.
Mwenyekiti Huyo Amesema Pembejeo Hizo Zimeanza Kusambazwa Kwenye Maeneo Ambayo Msimu wa
Mvua Huwahi, Vikiwemo Vijiji Vya Tarafa ya Igominyi Huku Akitaja Sifa za Watu Wanaostahili Kupata Pembejeo Hizo Kuwa ni Pamoja na Makundi Maalumu Wakiwemo Wazee na Walemavu, Watu Wanaosumbuliwa na Maradhi ya Muda Mrefu na Wenye Hali Duni ya Kimaisha.
Bi. Dumba Amezitaja Gharama za Pembejeo Hizo Ambapo Mbolea za Kupandia ni Shilingi Elfu 40 na Mbegu ni Shilingi Elfu 20Huku Serikali Ikichangia Shilingi Elfu 60 Kwa Jozi Hizo Mbili.
Ameongeza Kuwa Licha ya Vocha Hizo Kutokidhi Mahitaji Husika ya Wilaya Amewashauri Wananchi Kununua Pembejeo za Kilimo Kwa Mawakala na Maduka Yanayotambulika Kisheria na Kuendeleza Shughuli za Kilimo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment