Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Monday, October 21, 2013

RATIBA YA MUENDELEZO WA MICHUANO YA LIGI KUU YABADILIKA



KATIKA mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kwa wanawake chini ya miaka 20 Kanda ya Afrika kati ya Tanzania na Msumbiji itakayochezwa Oktoba 26,Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) limetangaza mabadiliko ya ratiba za michuano ya ligu kuu (VPL) Tanzania bara katika mechi zilizobakia.
Ofisa habari wa TFF Boniface Wambura amesema kuwa kutokana na mechi hiyo mabadiliko yataanzania katika mechi ya Oktoba 27 ambapo zitakutana timu ya Tanzania Prisons na Mbeya City na badala yake zitacheza Oktoba 29

.Mechi nyingine zilizobadilika ratiba ni zile ambazo zilitakiwa kucheza Oktoba 26 ambayo ni mechi ya Coastal dhidi ya Mtibwa sugar ambapo itachezwa Oktoba 28,na katika mechi za Oktoba 27 ambazo ni Simba itakayocheza na Azam,Ashant na Mbeya City ambazo zote zitacheza Octoba 28.

Katika mechi ambapo pia zilitakiwa kucheza oktoba 27 ni Rhino Rangers na JKT Ruvu pia Ashanti na Mbeya City ambapo zote zitacheza Oktoba 29.

Katika mechi ambazo zilitakiwa kucheza Oktoba 30 ni Coastal Union dhidi ya Mgambo Jkt,Prisons na Jkt Oljoro,Azam na Ruvu shooting,Mtibaw sugar na Rhino Rangers na Mbeya City dhidi ya Ashant united ambapo zote zitachezwa Novemba 2 na mechi ya Simba na Kagera sugar iliyotakiwa ichezwe Oktoba 30 itachezwa Oktoba 31

No comments:

Post a Comment