Mjasiliamali Mama Marieth Putika Mkoani Njombe Akihojiwa Juu ya Vipimo Kwenye Bidhaa Zake.
Na Gabriel Kilamlya Njombe.
Serikali Kupitia Wakala wa Vipimo Nchini Imesema Tatizo la Malalamiko ya Wafanyabiashara na Wakulima Mbalimbali Juu ya Vipimo Kwenye Mazao yao Linapaswa Kushughulikiwa Kwa Kushirikiana na Wananchi Wenyewe.
Akizungumza na Kituo Hiki Mkoani Njombe Afisa Vipimo Mkuu Kutoka Makao Makuu ya Wakala wa Vipimo Dar es Salaam Bi.Zainabu Kafungo Amesema Pamoja na Jitihada Kubwa Zinazofanywa na Serikali Juu ya Kudhibiti Tatizo la Vipimo Batili Ikiwemo Lumbesa Kwenye Zao la Viazi Mkoani Njombe Tatizo Hilo Linapaswa Kushirikiana na Wananchi Wenyewe.
Aidha Bi.Kafungo Ameeleza Kuwa Wakala wa Vipimo Tanzania Kwa Sasa Inaendelea na Ukaguzi wa Vipimo Vinavyotumika Katika Bidhaa Mbalimbali Pamoja na Kuwafikisha Kwenye Vyombo vya
Sheria Wale Wote Wanaokiuka Utaratibu wa Vipimo Kwenye Bidhaa Hizo.
Pamoja na Mambo Mengine Amesema Kuwa Ukaguzi Huo Unahusisha Mizani ya Vipimo yenye mhuri wa Serikali na Kwamba Mizani yote Inayokutwa Haina Muhuri wa Serikali Itakuwa Inafanya Kazi Kinyume Cha Sheria Hivyo Hatua za Kisheria Zinapaswa Kuchukuliwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment