MATUKIO ya mauaji ya kikatili yameendelea kushamiri mkoani Rukwa, baada ya watu wasiojulikana kumuua kikatili mtu mmoja kwa kumchinja na kutokomea kusikojulikana na kichwa cha mtu huyo.
Baadhi ya askari polisi wakitelemsha maiti ya mtu ambaye ameuawa kwa kukatwa kichwa na watu wasio fahamika na kutoweka na kichwa chake usiku wa kuamkia leo kwa ajili ya kuhifadhi katika hchumba cha kuhifadhia maiti kwenye hospitali ya mkoa iliyopo mjini Sumbawanga.
Mwenyekiti wa mtaa alipo kutwa marehemu alikuwa na haya ya kusema watu hao baada ya kufanya mauaji hayo walikwenda kumtupa kwenye eneo hilo ambapo asubuhi ya kuamkia leo ndio wiliwili wake ulibainika kuwepo hapo ukiwa hauna kichwa kwani waliondoka nacho ndipo yuliamuwa kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama.
Kwa upande wake, Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alisema kuwa polisi inaendelea kuwasaka watu waliohusika na tukio hilo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa
Kwa upande wake, Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alisema kuwa polisi inaendelea kuwasaka watu waliohusika na tukio hilo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa
No comments:
Post a Comment