Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Saturday, November 16, 2013

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYOJIRI KATIKA UPOKEAJI WA MWILI WA DK MVUNGI PAMOJA NA RATIBA YOTE YA MAZISHI



 Mwili wa Marehemu Dk. Sengondo Mvungi ukifanyiwa maombi mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.


 Wanachama wa NCCR-Mageuzi wakiwa wamelibeba sanduku lililohifandhi mwili wa kiongozi huyo wa NCCR-Mageuzi na Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya.


 Waombolezaji waliofika uwanjani hapo kuupokea Mwili wa Dk. Mvungi.


 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akiwa uwanjani hapo.


 Baadhi ya waombolezaji waliofika uwanjani hapo.


Mjane wa Marehemu, Bi Anna Mvungi akiwa uwanjani hapo kuupokea mwili wa mumewe




Ndugu wakilwa na masikitiko baada ya kumpoteza Dr.mvungi  



Mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya mabadiliko ya Katiba mpya na Mkurugenzi wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu wa NCCR-Mageuzi, Marehemu Dr.Sengondo Mvungi umewasili nchini kutoka Afrika Kusini.



Mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, ndugu jamaa na marafiki wa Marehemu Dr. Sengondo Mvungi walifika uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere upande wa Mizigo na kuupokea mwili wa kiongozi huyo na mwana familia.



Mapokezi ya mwili wa Dr. Mvungi aliyefariki juzi kufuatia majeraha ya shambulizi la majambazi lililomkuta nyumbani kwake November 2 mwaka huu na kupelekwa Nchini Afrika Kusini kwa Matibabu, yaliongozwa na Mkewe mama Anne Mvungi.



Viongozi wengine waliohudhuria ni pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba mpya, Jaji na Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Sinde Warioba, Waziri wa Uchukuzi.,Mwenyekiti wa NCCR-Magezi, na wajumbe takriban wote wa tume ya mabadiliko ya Katiba mpya.



Sanduku hilo lilifunikwa kwa bendera ya Chama cha NNCR-Magezi. 


Mwili wa marehemu Dk. Sengondo Mvungi unataraji kuagwa kesho katika viwanja vya Karimjee kabla ya kusafirishwa kwenda kijijini Kwao Kisangara juu, Wilaya ya mwanga mkoani Kilimanjaro kwa Maziko siku ya jumatatu.
__
RATIBA YA MSIBA WA DR.MVUNGI
______________
MUDA
TUKIO
JANA, NOVEMBA 15, 2013 – UWANJA WA NDEGE WA MWALIMU JK NYERERE
Saa 12:50 jioni
Kuwasili kwa mwili wa Marehemu – Uwanja wa Ndege wa Mwalimu JKN
LEO, NOVEMBA 16, 2013 – VIWANJA VYA KARIMJEE
Saa 2:00 – 3:30 asubuhi
Kuwasili kwa Wageni, Wananchi na Waombolezaji
Saa 3:30 asubuhi
Kuwasili Mwili wa Marehemu
Saa 4:00 – 5:45 asubuhi
Ibada ya Misa Takatifu, Viwanja vya Karimjee
Saa 5:45 – 6:55 mchana
Salaam za Rambirambi na Neno la Shukurani
Saa 6:55 – 8:40 Mchana
Kuaga Mwili wa Marehemu
Saa 9:00 Alasiri
Msafara kupeleka mwili wa marehemu Kibamba Msakuzi
KESHO , NOVEMBA 17, 2013 – NYUMBANI KWA MAREHEMU - KIBAMBA, MSAKUZI
Saa 2:30 – 4:30 asubuhi
Ibada ya Misa nyumbani kwa marehemu
Saa 5:00 asubuhi
Kuanza safari ya kwenda Chanjale, Kisangara Juu, Mwanga, Kilimanjaro

No comments:

Post a Comment