Mahakama ya Mwanzo ya Mjini Lindi ambayo ilitoa hati ya wito wa mahakama kwa mmoja wa wafanyabiashara kuja kujibu  shitaka
Waafanyabiashara
 waliokusanyika Mbele ya Mahakama Ya Mwanzo ya Mji wa lindi, wakisubiri 
kujua hatma ya mfanyabiashara mwenzao aliotakiwa na mahakama siku hii ya
 leo
Akinamama
 hawakuwa nyuma nao waliungana na wenzao katika kuhakikisha wanajua kila
 nyendo inayo kwenda, wakiwa nje ya Mahakama ya Mwanzo
Wakati
 huo Maduka na Masoko yote Mjini hapa Yalikuwa yamefungwa na Baadhi ya 
wafanyabiashara wakiwa nje ya Soko kuu na kupanga Biashara zao nje ya 
Soko kama inavyoonekana pichani.
Baadhi ya Wananchi wakiendelea kupata Huduma hafifu katika soko kuu Mjini Lindi kufuatia mgomo wa Wafanyabiashara wa Mji huu.
Mandhari
 ya Mji Leo asubuhi ukionekana hivi ukiwa hauna pilika pilika za watu 
kufuatia mgomo wa wafanyabiashara, Maduka na Masoko na Stationary zote 
zimefungwa hakuna huduma inayotolewa na wafanyabiashara wako katika 
Mahakama Ya mwanzo kujua hatma ya Mfanyabiashara mwenzao pamoja na Mambo
 mengine wanayo yalalamikia kuhusiana na Kodi mbalimbali
 Chanzo: Lindi yetu
No comments:
Post a Comment