
Shirika
la ndege la Auric Air mwishoni mwa wiki limefanikiwa kuzindua safari
safari za kila siku za ndege kati ya Morogoro na Dar es salaam ikiwa
ni katika utekelezaji wa ahadi yake katika kuchangia maendeleo ya
sekta ya usafiri wa anga nchini.
Katika
uzinduzi huo ambao mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro
Joel Bendera ambaye anaelezea kuzinduliwa kwa safari hizo kutasaidia
kuukuza mji wa Morogoro kiuchumi, kupitia sekta ya utalii, na
hatimaye kuongeza kasi ya mikakati iliyopo ya kuufanya mji huo kuwa
jiji.
“Ni fursa sasa kwa wananchi wa morogoro kukuza
biashara zao
Kutokana na kurahisishwa mawasiliano kati ya mikoa
hiyo miwili, na hata
Wagonjwa kufuata kwa haraka huduma za rufaa
na kitabibu” anasema Bendera.
Auric Air katika taarifa yake
kwenye mtandao wa facebook imeeleza wazi lengo la kuzindua kwa safari
hizo kuwa pamoja na kuukuza uchumi pia itachochea maendeleo ya mkoa
kwa ujumla.
“Tuta
safiri kila siku,kuondoka morogoro saa 12:30 (alfajiri) asubuhi na
kutoka dar es salaam saa 11:15 jioni kwa kutumia ndege yetu yenye
uwezo wa kubeba habiria 13 kwa safari moja ambapo safari hiyo
itachukua dakika 35” inaeleza taarifa hiyo
Shirika hilo
linasema limejipanga mathubuti katika safari hizo na kuahidi kutoa
huduma hiyo kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zote ili
kuendeleza sifa yake ya kuwa shirika lenye huduma bora za usafiri wa
anga nchini.
Auric
Air pia inatarajia kuongeza safari zake kutoka Dar es salaam, kupitia
Ifakara hadi Songea kwa kwa lengo la kuwafikishia huduma hiyo
watanzania katika mikoa yote.
Tazama
picha zaidi za uzinduzi ulivyokuwa
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera akishuka kwenye ndege ya Auric Air
wakati wa uzinduzi wa safari za ndege kati ya Dar es Salaam na Morogoro
Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo akipanda kwenye ndege ya Auric Air
Tabianch blog
No comments:
Post a Comment