Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Friday, December 6, 2013

MAISHA YA NELSON MANDELA ENZI ZA UHAI WAKE VYOTE HAPA

Miaka ya Mapema

1952




Kesi ya Uhaini

1956

Mandela alifuzu kama wakili na kuanzisha kampuni ya kwanza ya sheria inayomilikiwa na mtu mweusi mwaka 1952 na kuiendesha kwa ushirikiano na Oliver Tambo, na kutoa huduma za kisheria kwa wale ambao walikosa uwakilishi. Akihofiwa kupigwa marufuku na serikali ya ubaguzi wa rangi, ANC ilimtaka Mandela kuhakikisha kuwa chama hicho kinaweza kuendesha harakati zake kimya kimya. Alikamatwa mwaka 1956 na kufunguliwa mashtaka ya uhaini yeye pamoja na wenzake 155. Baada ya kesi yake iliyochukua miaka minne, ilitupiliwa mbali . Mnamo mwaka 1958, Mandela alimuoa Winnie Madikizela.

Kufungwa Maisha

1964

Sheria ya hali ya hatari ilitangazwa baada ya polisi kuwaua waandamanaji 69 mjini Sharpville mwaka 1960. Serikali ilihofia kuwa wangelipiza kisasi na hivyo kuharamisha chama cha ANC. Chama hicho baadaye kiliendesha harakati zake za kijeshi kichinichini wakiongozwa na Mandela.Mwaka 1962, Mandela alikamatwa kwa kosa la kuondoka nchini bila kibali. Wanachama wengine wa ANC walikamatwa. Akiwa jela Mandela alishtakiwa kwa kosa la hujuma. Yeye na wengine saba walihukumiwa jela katika kisiwa cha Robben mwaka 1964

Huru hatimaye

1990

Jamii ya kimataifa iliiwekea vikwazo zaidi serikali ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini. Vikwazo vya kwanza viliwekwa mwaka 1967.Shinikizo zilizaa matunda na mnamo mwaka 1990, rais FW De Klerk akakiondolea marufuku chama cha ANC. Tarehe 11 Februari, Mandela aliachiliwa baada ya miaka 27 jela. Umati wa watu ulimshangilia huku yeye pamoja na mkewe wakiondoka sehemu ya jela. Katika mkutano wa kwanza wa chama cha ANC mwaka uliofuata, Mandela alichaguliwa kama kiongozi wa chama .Mazungumzo yakaanza ya kuunda serikali ya pamoja ya waafrika weusi na wazungu.

Tuzo ya amani ya Nobel

1993

Mnamo mwaka 1993, Mandela na rais wa nchi hiyo wakati huo, walituzwa tuzo ya amani ya Nobel kwa juhudi za kuleta uthabiti Afrika Kusini. Akikubali tuzo hiyo, Mandela alisema kuwa '' tutafanya kila tuwezalo kuweza kuleta mageuzi duniani.'

Rais mpya

1994

Mnamo mwaka1994,kwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika Kusini, watu wa rangi zote walipiga kura katika uchaguzi huru na wa kidemokrasia. Mandela alichaguliwa. Akihutubia umma, katika sherehe ya kuapishwa kwake, tarehe 10 mwezi Mei, mwaka 1994, alisema: "uhuru utawale, Mungu aibariki Afrika!'' Tatizo lake kubwa lilikuwa ukosefu wa nyumba za kutosha kwa watu maskini na mitaa ya mabanda iliendelea kuongezeka.Thabo Mbeki alichukua uongozi wa nchi huku Mandela akiuza sera za nchi hiyo kimataifa.

Akitoka Robbben

1995

Kuadhimisha miaka mitano baada ya kuachiliwa kwake, Nelson Mandela alizuru kisiwa cha Robben mwezi Februari mwaka 1995 alikozuiliwa kwa miaka 18. Ziara yake ilikuwa mwaka 1956 mwezi Februari pamoja na wafungwa wenzake waliowahi kufungwa kisiwani humo na kufanya kazi ngumu. Mapafu ya Mandela yanasemekana kuathirika alipokuwa anafanya kazi katika machimbo ya mawe.

'Usiniite''

2004

Thabo Mbeki alichukua mamlaka kutoka kwa Mandela kama  kiongozi wa chama tawala ANC na hata kushinda uchaguzi wa mwaka 1999.Mandela alimuoa Graca Machel, mjane wa aliyekuwa rais wa Msumbiji, akiwa na miaka 80. Aligunduliwa kuwa na saratani ya Tezi Kibofu na hivyo kuanza matibabu.Mnamo mwaka 2004, alitangaza kujiuzulu, akisema kuwa anataka maisha ya kimya nyumbani kwake na familia yake. Kwa mzaha aliwaambia wandishi wa habari wasimpigie simu.

Sherehe ya siku ya kuzaliwa kwake

2008

Wanamuziki, waigizaji na wanasiasa waliungana na Mandela  katika sherehe kubwa uwanja wa Hyde Park mjini London kusherehekea miaka 90 ya kuzaliwa kwake. Akiongea na wale waliofika, aliwaambia, ''ni wakati kwa kizazi kipya kuchukua uongozi, kibarua kwenu sasa.''

Kuugua

2010

Mandela aliweza kuonekana hadharani mara kadhaa baada ya kustaafu. Ingawa alionekana katika sherehe ya kukamilika kwa dimba la kombe la dunia mwaka 2010 nchini humo. Januari mwaka 2011, alilazwa hospitalini kwa ukaguzi maalum, huku serikali ikiwakumbusha watu kuwa aliwahi kupata matatizo ya kupumua. Alipokea matibabu ya ugonjwa wa mapafu mwaka 2012 na pia mwaka 2013 .


ubondia na mandela

Hata wakati yupo kifungoni katika chumba chake kidogo cha gereza katika kisiwa cha Robben, Nelson Mandela alifanya mazoezi kujiweka fiti kiafya na mwili na akili.


Enzi za ujana wake alipata kuwa bondia wa uzani wa juu (Heavyweight), kama ambavyo anaonekana katika picha kadhaa akijifua.

Mandela pia alikuwa akijifua na swahiba wake na bondia wa uzito wa kati Jerry Moloi ambaye yeye ngumi kwake ilikuwa ni kazi na sehemu ya maisha yake kwani rekodi yake inaonyesha kushinda mabambano 13, kupoteza 15 na kutoka sare 30.

Picha hii wakiwa juu ya jengo mjini Johannesburg.
Sanamu hii ya Nelson Mandela iliyotokana na picha hiyo hapo juu ikiwa imewekwa mtaani kumuenzi Bondia huyo mpigania uhuru wa Afrika Kusiani.


Katika kitabu chake mzee Nelson Mandela alicho anza kukiandika akiwa gerezani cha, Safari ndefu ya Uhuru (Long Walk to Freedom), Mandela anaelezea upendo wake katika mchezo wa ngumi wa ndondi (na kwa nini alifanya hivyo):

“Mimi sikuwa na furahia mapambano uliongoni katika ngumi sana kama sayansi ya yake inavyosema. Mimi nilikuwa navutiwa na jinsi mtu anavyouongoza mwili kujikinga, na vile mwingine akitumia mkakati wa kushambulia na kurui nyuma ili kupata ushindi katika mchezo”, aliandika Mandela.

Ngumi ni usawa katika ulingo, lakini cheo, umri, rangi, na mali ni vitu visivyo na maana. Mimi kamwe sijafanya mapigano yoyote halisi baada ya mimi kuingia katika siasa. 

Madhumini yangu makubwa yalikuwa katika mafunzo; mazoezi ya ngumi yalinifanya kupiteza msongo wa mawazo. Baada ya ya mazoezi ya jioni nilijihisi kiakili na kimwili ni mwepesi.
 
Nelson Mandela akirusha ngumi kwa Bigwa wa Masubwi wa zamani Duniani Mohamed Ally.

Nelson Mandela akiweka paling na Mkali wa ngumi duniani Lennox Lewis.

Nelson Mandela akiwa na Mkali wa ngumi duniani Mike Tyson.


No comments:

Post a Comment