Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Tuesday, December 10, 2013

Vigogo watakaomuaga Mandela leo hawa hapa

 DUNIA leo inaelekeza macho na masikio Afrika Kusini, wakati viongozi 90 wakuu wa nchi na Serikali, viongozi wa mashirika ya kimataifa na watu mashuhuri, watakaposhiriki katika siku ya kitaifa ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Rais wa Kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.
Jana jioni Serikali ya Afrika Kusini ilitoa orodha ya majina ya watu zaidi 90, kutoka kila pembe ya dunia watakaohudhuria mazishi hayo, akiwemo Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete.
Wakati majina hayo yakitolewa, hoteli za kifahari katika mji wa Sandton, Johannesburg Afrika Kusini, zilitoa taarifa kwa wateja wake kuondoka vyumbani kupisha ugeni huo mkubwa kuwahi kuonekana katika nchi moja Afrika.
Viongozi hao mbali na Rais Kikwete ni pamoja na Rais wa Afghanistan, Hamid Karzai, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Dk Nkosazana Dlamini-Zuma na Spika wa Bunge la Algeria, ambaye ni mkubwa kuliko Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Abdelkader Bensalah.
Wengine ni Makamu wa Rais wa Angola, Manuel Vicente, Waziri wa Umoja wa Mataifa ya Kiarabu, Amb Samir Hosny, Kaimu Rais Argentina, Amado Boudou na Waziri Mkuu wa Australia, Tony Abbott.
Pia yumo Waziri Mkuu Bahamas, Perry Christie, Rais wa Bangladesh, Abdul Hamid, Mfalme Philippe wa Ubelgiji, Rais wa Benin, Boni Yayi, Rais wa Botswana, Luteni Jenerali, Seretse Khama Ian Khama na Rais wa Brazil, Dilma Rousseff.
Burundi itawakilishwa na Rais Pierre Nkurunziza, na pia atakuwepo Waziri Mkuu wa Canada, Stephen Harper, Rais wa Chad, Idriss Déby Itno, Rais wa China Li Yuanchao na Makamu wa Rais wa Jumuiya ya Madola, Kamalesh Sharma Nchi ya Comoro itawakilishwa na Rais wake, Ikililou Dhoinine ambapo pia atakuwepo Rais wa Jamhuri ya Kongo, Denis Sassou-Nguesso, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila na Rais wa Ivory Coast, Allassane Ouattara.
Wengine ni Rais wa Croatia, Ivo Josipovic, Rais wa Cuba, Raúl Castro, Mtoto wa Mfalme wa Denmark, Prince Federick, Rais wa Djibouti, Ismaïl Omar Guelleh na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Ato Hailemariam Desalegn.
Mazishi hayo pia yatahudhuriwa na Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Mbasogo, Rais wa Baraza la Ulaya, Herman van Rompuy, Rais wa Ufaransa, François Holland, Rais wa Finland, Sauli Väinämö Niinistö na Rais wa Ghana, John Mahama.
Nchi ya Guyana itawakilishwa na Rais Donald Ramotar na pia atakuwepo Rais wa Gabon, Ali Bongo Ondimba, Rais wa Ujerumani, Joachim Gauck, Kiongozi wa Ufalme wa Luxembourg, Henry wa Luxembourg na Rais wa Guinea, Profesa Alpha Condé.
India itawakilishwa na Rais Pranab Mukherjee na pia atakuwepo Rais wa Ireland, Michael Higgins, Waziri Mkuu wa Italia, Enrico Letta, Mtoto wa Mfalme wa Japan, Prince Naruhito, Waziri Mkuu wa Jamaica, Portia Miller.
Pia yupo Malkia wa Jordan, Rania Al Abdullah atakayefuatana na Waziri Mkuu wake, Dk Abdullah Ensour, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Waziri Mkuu wa Korea Kusini, Hongwon Chung na Waziri Mkuu wa Lebanon, Najib Mikati.
Lesotho itawakilishwa na Waziri Mkuu wake, Thomas Thabane ambapo pia atakuwepo Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, Rais wa Mauritania, Mohamed Ould Abdel Aziz, Waziri Mkuu wa Mauritius, Dk Navinchandra Ramgoolam na Rais wa Malawi, Joyce Banda.
Mexico itawakilishwa na Rais Peña Nieto, ambapo pia atakuwepo Rais wa Msumbiji, Armando Guebuza, Rais wa Namibia, Hifikepunye Pohamba, Waziri Mkuu wa New Zealand, John Key, Rais wa Niger, Mahamadou Issoufou, Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan na Mtoto wa Mfalme wa Norway, Prince Haakon.
Pia atakuwepo Rais wa Pakistan, Mamnoon Hussain, Rais wa Mamlaka ya Palestinian, Mahmoud Abbas, Rais wa Ureno, Aníbal Cavaco Silva, Rais wa Jamhuri ya Sahrawi, Mohamed Abdelaziz na Mtoto wa Mfalme wa Saudi Arabia, Muqrin bin Abdulaziz Al-Saud.
Senegal itawakilishwa na Rais Macky Sall, Serbia atakuwepo Rais Tomislav Nikolić. Wengine ni Rais wa Ushelisheli, James Michel, Rais wa Slovenia, Borut Pahor na Rais wa Sudan Kusini, Jenerali Salva Kiir.
Hispania itawakilishwa na Mtoto wa Mfalme, Felipe de Borbón, ambapo pia atakuwepo Rais wa Sri Lanka, Mahinda Rajapaksa, Rais wa Surinam, Desiré Bouterse, Waziri Mkuu wa Swaziland, Dk Sibusiso Dlamini na Waziri Mkuu wa Sweden, Fredrik Reinfeldt.
Wengine ni Rais wa Uswis, Ulrich Maurer, Rais wa Gambia, Profesa Yahya Jammeh, Waziri Mkuu wa Timor ya Mashariki, Rala Xanana, Waziri Mkuu wa Trinidad na Tobago, Kamla Persad-Bissessar na Rais Tunisia, Mohamed Moncef Marzouki.
Uganda itawakilishwa na Rais Yoweri Museveni, ambapo pia atakuwepo Waziri wa Utamaduni kutoka Falme za Kiarabu, Mtoto wa Mfalme wa Uingereza, Prince Charles na Waziri Mkuu wake David Cameron, Rais wa Marekani, Barack Obama, Rais wa Venezuela, Nicolás Moros, Rais wa Zambia, Michael Satan na Rais, wa Zimbabwe, Robert Mugabe.

No comments:

Post a Comment