Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Monday, December 30, 2013

WATUPWA JELA MIAKA (40) KAKA NA MDOGO KWA UJANGILI

 Mahakama ya wilaya ya bariadi mkoani simiyu imewahukumu watu wawili kutumikia kifungo cha miaka 40 jela au kulipa faini mil30 baada ya kupatikana na kosa la kufanya ujagili katika hifadhi ya taifa ya maswa.

Waliokumbwa na hukumu hiyo ni Mandago Say (58) na Feya Say (64) wote wakazi wa wilayani meatu mkoani hapa.

Hukumu hiyo imetolewa na hakimu wa mahakama ya wilaya hiyo Robart Oguda baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.

Awali ilidaiwa na mwendesha mashitaka wa polisi Inspekta Samweli Kilabuko kuwa watuhumiwa walitenda kosa hilo april mwaka huu kwa kuingia katika hifadhi ya taifa ya maswa na kuwinda bila ya kuwa na kibali.

Na kuwauwa wanyama wawili ambao ni  swala na nyati wakiwa na gharama ya zaidi ya mil 9 kwa kutumia silaha.

No comments:

Post a Comment