Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Wednesday, January 29, 2014

AMANI YATOWEKA TARIME, WALIOUWAWA NA JAMBAZI WAFIKA SABAAMANI YATOWEKA TARIME, WALIOUWAWA NA JAMBAZI WAFIKA SABA

HALI ya usalama Tarime imezidi kutoweka baada ya Jambazi lisilofahamikalikiwa na bunduki  ambayo haijafahamika aina yake   kuendelea kuuwa watu kwa risasi katika mazingira tofautitofauti ambao ni jinsia ya kiume na idadi ya waliouwawa kufikia saba hadi sasa na inadaiwa uuwa watu na kupotea bila kutambuliwa.

Jambazi hilol isilofahamika  watu nausiku wa saa mbili januari   27 /2014  maeneo ya Nkende limemuuwa mwendesha bodaboda Juma Marwa Mkazi wa Nkende mjini Tarime akiwa anaelekea Nyumbani kwake amabye alikufa akiwa hospitali akipatiwa matibabu.

Mganga wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji Tarime Marco Nega amesema kuwa  tangu January 27  hadi sasa hospitali imeendelea kupokea watu waliouwawa na majeruhi ambao wamefanyiwa uchunguzi na kugundulika wakiwa wamejeruhiwa kwa risasi katika sehemu mbalimbali za mwili nakwamba watu wapatao 7 wamekufa.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya Justus Kamugisha  amesema wamemkamata mtu mmoja anaeshukiwa amabaye yuko chini ya ulinzi kwa mahojiano nakwamba anazidi kuongeza vikosi vya doria kuimarisha ulinzi na usalama Tarime

No comments:

Post a Comment