
Wilaya ya chunya
- wizi wa gari.
Mnamo tarehe 06.01.2014 majira ya saa
15:00hrs huko eneo la kuegesha magari ya
Kampuni ya Sunshine Mining LTD katika kijiji cha Matundasi, kata ya Matundasi,
tarafa ya Kiwanja,
Wilaya ya Chunya mkoa wa Mbeya. Msabaha
s/o Rashid Kafulama, fundi mkuu wa
kutengeneza magari wa Kampuni hiyo aliiba
gari lenye nambari za usajili T 421 CHG aina ya
Toyota L/Cruiser ingle cabin rangi nyeupe chases no JCLB-715407036705
lenye thamani ya USD 35,000 na kwenda
mahali kusikojulikana. Mbinu ni kujaribu
kuendesha gari hilo baada ya kulifanyia
matengenezo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ahmed Z. Msangi anatoa
wito kwa yeyote mwenye taarifa juu ya
mahali alipo mtuhumiwa pamoja na gari azitoe katika mamlaka husika ili
akamatwe na sheria ichukue mkondo wake,vinginevyo ajisalimishe mwenyewe.
Wilaya
ya Mbarali - Ajali ya
Moto.
Mnamo tarehe 06.01.2014 majira ya saa
20:15hrs huko katika Shule ya
Wasichana ya Sekondari Igumbilo
inayomilikiwa na Kanisa la Lutherani, iliyopo
kata ya Chimala, tarafa ya Ilongo wilaya ya Mbarali
mkoa wa Mbeya. bweni moja la shule hiyo liliungua moto na kuteketeza mali zote zilizokuwa ndani ya bweni hilo. chanzo bado kufahamika, ingawa uchunguzi wa awali unaonyesha ni
hitilafu ya umeme. hakuna madhara
ya kibinadamu yaliyotokea. thamani
halisi ya mali iliyoteketea bado
kufahamika. Kamanda wa Polisi mkoa wa
Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Polisi Ahmed Z. Msangi anatoa wito kwa jamii kuwa makini na kuchukua
tahadhari dhidi ya majanga ya moto.
Wilaya
ya Mbeya Mjini – kupatikana na pombe haramu ya
moshi
[gongo].
Mnamo tarehe 07.01.2014 majira ya saa 12:50hrs huko katika kilabu cha pombe
za kienyeji cha Mponzi kilichopo
kata ya Kagera, tarafa ya Sisimba jiji na mkoa wa Mbeya. Askari Polisi wakiwa doria /msako
walimkamata Prisca d/o Godwin, miaka
27, Kyusa, Mkulima, mkazi wa mtaa wa Kagera
akiwa na pombe haramu ya moshi
[gongo] ujazo wa lita 1.5. mtuhumiwa
ni mtumiaji na muuzaji wa pombe hiyo. taratibu zinafanywa ili afikishwe
Mahakamani. Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Polisi Ahmed Z. Msangi anatoa wito kwa
jamii kuacha kutumia pombe haramu ya
moshi[gongo] kwani ni kinyume cha sheria na ni hatari kwa afya ya mtumiaji.
signed
by:
[Ahmed Z. Msangi -SACP].
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya.
No comments:
Post a Comment