Mji wa Zanzibar
Polisi Visiwani Zanzibar wamethibitisha kutokea milipuko mitatu ya mabomu kati ya Jumapili na Jumatatu leo mchana visiwani humo.
Akizungumza na wandishi wa habari , mkuu wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame amesema milipuko
miwili imetokea leo katika eneo la mgahawa wa Mercury huku mlipuko
mwingine ukiwa umetokea katika eneo la Mkunazini, ikifuatia mlipuko
uliotokea jana Jumapili katika eneo la Pangawe.
Mkuu huyo wa Polisi Zanzibar amesema kuwa hakuna
vifo wala majeruhi katika matukio yote matatu wala mali iliyoharibiwa,
isipokuwa madhara ya kisaikolojia kutokana na hofu na taharuki kutokana
na matukio hayo.
Aidha mkuu huyo wa Polisi ameeleza kuwa upelezi
unaendelea ili kuwabaini waliohusika katika matukio hayo ingawa hadi
wakati huu hakuna mtu au mshukiwa yeyote aliyekwishamatwa kuhusiana na
matukio hayo.
Kuhusu hatua za tahadhari kufuatia matukio hayo
Kamanda Makame amesema Polisi wanaendelea kuimarisha ulinzi katika
sehemu mbali mbali visiwani humo ikiwa ni pamoja na kufanya doria katika
maeneo kadhaa na amewaondoa hofu wananchi wa visiwa hivyo kuhusu
usalama wao.
Chanzo;BBC swahili
No comments:
Post a Comment