Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Wednesday, March 19, 2014

HOI KWA KUNYWESHA DAWA YA KUBAINI WEZI

PENDO Kona, amepoteza fahamu na kulazwa katika hospitali ya DDH-Bunda, akidaiwa kunyweshwa dawa inayosadikika kuwa sumu na waganga wakienyeji.Mwanamke huyo mkazi wa Bunda, anadaiwa kunyweshwa dawa hiyo ili awabaini wezi wa ng’ombe wake.Pendo inasemekana aliibiwa ng’ombe wawili Januari mwaka huu, na aliamua kwenda kwa waganga wa kienyeji ili asaidiwe kuwapata wezi wake.Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, Fredinand Mtui, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 3:00 asubuhi, katika kijiji cha Mugeta, wilayani Bunda.Kamanda Mtui, alisema watu hao waliojiita waganga wa kienyenyeji, waliwanywesha wanafamilia hao watatu, ili wawabaini wezi wa ng’ombe wawili, mali ya Pendo walioibiwa mwishoni mwa Januari, mwaka huu.Kamanda Mtui, alisema mwanamke huyo alipokunywa dawa hiyo, aliishiwa nguvu na kupoteza fahamu ambapo alipelekwa  katika hospitali ya DDH-Bunda kwa matibabu.Hata hivyo, alisema Polisi wanamshikilia kijana mmoja ambaye ni mtoto wa mke mwenzake na Pendo, kwani ndiye anayetuhumiwa kuwaleta waganga hao waliotoroka baada ya tukio.

No comments:

Post a Comment