Huu ni mfereji wa kupitisha maji taka ambao unao tumika katika Hospitali ya Palestina ambapo ulizidiwa kwa kujaa maji na hatimaye kufumuka na kusababisha kusambaa kwa maji machafu katika kila kona ya Hospitali hiyo
Mmoja wa wagonjwa akiwa anangojea kupata huduma baada ya mvua hiyo kubwa kuisha
Haya ni maji machafu ambayo yametapakaa sehemu ya mbalimbali ya hospitali
Kushoto ni Mgonjwa akiwa amelala juu ya Benchi ambapo pembeni kuna maji na matope
Hii ndio hali halisi ya mifereji iliyopo katika ya Hospitali ya Sinza Palestina
sehemu ya kuingilia katika hospitali hiyo
Wagonjwa zaidi wakingojea vyumba visafishwe ili kuweza kuendelea kupatiwa huduma
Moja ya Chumba ambacho kilikuwa kimejaa tope kikingojea kusafishwa
sehemu ya kupumzikia wagonjwa
Baadhi ya viti vikiwa vimeegeshwa kwa ajili ya kungoja kufanya usafi
Hakuna mtu katika maeneo haya kutokana na mvua kubwa iliyonyesha na kuharibu mazingira hayo
Kila kitu kimekaa hovyo hovyo baada ya mvua kubwa hiyo kunyesha
Baadhi ya vifaa vya kutibia wagonjwa vikiwa juu ya moja ya kitanda cha kutibia wagonjwa huku watu wakingoja huduma ya matibabu.
Huu ndio Mtaro wa maji machafu ambapo maji kutoka nje yamepita ndani ya hospitali hiyo na kusababisha maafa baada ya Mtaro huo kuziba.
Mapema mchana wa leo kumetokea mvua kubwa katika maeneo mbalimbali ya Jijini Dar es salaam kumesababisha usumbufu mkubwa baada ya maeneo mengi kukumbwa na tatizo la maji mengi ambayo yaliziba barabara , nyumba za watu pamoja na maeneo mbalimbali.
Mvua hizo kubwa ambazo hata mamlaka ya hali ya hewa wametahadhalisha kwamba zitakuwepo kuanzia Tarehe 5.03.2014 hadi Tarehe 7.03.2014 zimesababisha usumbufu mkubwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Kinondoni Sinza - Palestina kujaa maji kila kona na kupelekea wauguzi kuacha kazi na kupanda juu ya Meza na viti wakikwepa maji hayo. Na wengine kukimbia katika eneo hilo kuhofia maji hayo.
Walikwepa maji hayo kutokana na kwamba si ya mvua tuu lakini yalikuwa ni Machafu yaliyochanganyikana na maji kutoka vyooni ambapo kuna chemba moja ya maji machafu imepita hapo.
Baada ya mvua hiyo kwisha iliwalazimu wafanya usafi wachukue muda wa zaidi ya dakika 30 kufanya usafi na kutoa matope yaliyokuwa yamejaa kila chumba.
Akiongea kwa Simu Mganga Mkuu wa Hospitalu hiyo amekili kwamba kuna usumbufu mkubwa wa chemba hiyo na mvua hasa katika kipindi hicho ambapo zinanyesha kwa kiasi kikubwa.
Ameongeza kwa kusema kwamba kunajuhudi zinahitajika kufanyika ili kuweza kunusuru tatizo hilo lisiendelee.
Nao baadhi ya wagonjwa ambao wengine walikuwa katika hali ambayo si nzuri wamesema wanaiomba serikali itazame tatizo hilo maana licha ya maji hayo kuwa mengi lakini pia ni hatari kwa afya zao kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment