

Wananchi
wa kijiji cha Ilandutwa,kata ya Mgama,Iringa Vijijini wakinyanyua
mikono yao juu kumuunga mkono Mgombea Ubunge jimbo la kalenga,Ndugu.
Godfrey Mgimwa.

Wananchi
wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni wa CCM,kwa ajili
kuzisikiliza sera za mgombea Ubunge wa Jimbo la kalenga,Ndugu Godfrey
Mgimwa,uliofanyika kwenye kijiji cha Ilandutwa,kata ya Mgama Iringa
Vijijini

Mgombea
ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia chama cha Mapinduzi CCM Bw. Godfrey
Mgimwa akiwahutubia wananchi katika kijiji cha Ilandutwa kata ya Mgama
Iringa vijijini akiendelea na mikutano mbalimbali ya kampeni ambapo
amewaomba wananchi wa vijiji hivyo kumkopesha imani yao na kumpa kura za
ndiyo siku ya machi 16 jumapili ijayo ili aweze kuwalipa maendeleo
katika jimbo hilo.

Wananchi wakishangilia jambo

Diwani wa kata ya Mgama Bw. Denis Lupala akipiga magoti kumuombea kura mgombea wa CCM Bw. Godfrey Mgimwa.

Wakazi
wa kijiji cha Itwanga,Kata ya Mgama wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri
kwenye mkutano huo wa kampeni,ambapo siku ya jumapili machi 16 ndio
utafanyika uchaguzi mdogo wa kumpata Mbunge wa Jimbo la Kalenga.


Wakazi
wa kijiji cha Udumka,kata ya Ifunda Iringa Vijijini wakimsikiliza
mgombea Ubunge wa jimbo la kalenga,Godfrey Mgimwa akinadi sera zake na
kuomba kupigiwa kura za kutosha na hatimae kuibuka na ushindi wa
Ubunge,ili apate ridhaa ya kuwaongoza na kuyaendeleza yale yaliyoachwa
na Mbunge aliyepita,Marehemu William Mgimwa.

Mgombea
ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia chama cha Mapinduzi CCM Bw. Godfrey
Mgimwa akiwahutubia wananchi katika kijiji cha Udumka Kata ya Ifunda,
Iringa vijijini mapema leo jioni..

Baadhi ya Wanahabari wakiendelea kuchukua matukio mbalimbali yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo
chanzo;jiachie blog
No comments:
Post a Comment