Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Mwakikonge, wilayani
Mkinga wanasomea chini ya miti ya mikorosho kutokana na kukosekana kwa
madarasa shuleni hapo.
Shule hiyo yenye wanafunzi 450 ina madarasa mawili, walimu wanne na
haina nyenzo muhimu za kufundishia tangu ilipoanzishwa mwaka 2009.
Akizungumza katika mahojiano na NIPASHE, Diwani wa Kata ya Duga, Ali
Ali, alisema wanafunzi wa shule hiyo walianza kusoma chini ya mti na
mpaka sasa wanafunzi wa darasa la kwanza mpaka la tano wanasoma chini ya
mti na darasa la sita na la saba tu ndio waliopo madarasani.
“Hii shule inakabiliwa na changamoto nyingi sana ikiwamo ukosefu wa
madarasa na walimu….walimu waliopo ni wanne tu na madarasa ni mawili tu
na mwaka huu tuna wanafunzi wa darasa la saba tangu shule ilipoanzishwa
hatujui matokeo yatakuaje," alisema Ali. (UNAWEZA KUCHUKUA HII KAMA
QUATATION)
Hata hivyo, wananchi wa Sweden kupitia mfuko wa Agape Charity, wametoa
msaada wa vitabu vya masomo mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh.
milioni 6.8.
Mwakilishi wa Agape ni kwamba Charity, Clemeny Hongole, alisema vitabu
hivyo ni vya masomo ya Kiswahili, Historia, Jiografia, Uraia, Stadi za
kazi na kiongozi cha mwalimu kwa masomo yote.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment