Kulia ni Magari mbalimbali ya Serikali yakiwa yamepaki eneo la Mwenge wakai zoezi la ubomoaji likiendelea
Hili ni eneo la ndani ya Mwenge ambapo limebomolewa vibanda vyote
Akina Mama eneo la Mwenge ndani
kiasi wakiwa wanahaha huku wahangaika kutoa vitu vyao baada ya Bomoa Bomoa kupita... Hawa ni wale wauza Chai na Supu asubuhi
Huwezi amini lakini ndio hali halisi sasa eneo jirani na Kituo cha Mabasi Mwenge hakuna tena Adha ya vibanda , lakini umebaki uchafu uliopitiliza na kugundulika kuwa hawa watu walikuwa wakifanya Biashara katika maeneo ambayo si salama
Hili ni eneo ambalo lilikuwa ni Maarufu kwa ajili ya kuuza vitu mbalimbali kama mitumba na viatu lakini kwa sasa hakuna kitu ni peupe
Huu ni uchafu uliopitiliza
wakiendelea kukusanya mabaki ya Mabanzi katika eneo hilo la mwenge
Kwa wale akina dada hili lilikuwa eneo maarufu sana kwa ajili ya Kutengenezea nywele na saloon bubu ambazo zote zimevunjwa vunjwa kwa sasa
Hapa juu mwanzo kulikuwa na mabanzi ya kutosha na wakina dada wengi walikuwa wanapenda kuwa hapa wakitengenezwa nywele zao wasijue kuwa walikuwa wakikaa katika eneo chafu kama hili.
Gari hili likijiandaa kuondoka baada ya somba somba
Kwa kuliangalia Eneo hili utasema ni chafu sana lakini ndio ambalo lilikuwa maarufu hasa kwa akina mama na akina dada kutengenezea kucha zao na kusuguliwa miguu, Je kama wangejua ni pachafu hivi wangeweza kugusa hata kuja kutengeneza kucha?
Bomoa bomoa ikiendelea
Baada ya kufanya manunuzi watu hutupa takataka tuu, zilikuwa zikijificha kulingana na mkusanyiko wa watu lakini hii ndio hali halisi sasa
Hakuna Vibanda lakini adha imebakia sasa ni ya uchafu
Je hapa tutapona magonjwa ya mlipuko?
Peupe hata kuna nafasi ya kutembea kwa miguu
Huu ni upande wa pili wa kuelekea Mikochemi ambapo bajaji Hupaki napo wamesafisha kwa kubomoa vibanda vyote hapa ni Shwari peupe
Picha hizi mbili ni eneo maarufu sana ambapo watu walikuwa wanauza Vifaa vya umeme na DVD, Sub Woofer pamoja na Radio bila kusahau TV sasa pamebaki kama hivi, Je walikuwa hawajui kama ni pachafu kiasi hiki?
Mgambo wakiwa wamemaliza kazi yao hapa ......
Picha na Pamoja Blog/ Dar es salaam yetu Blog
No comments:
Post a Comment