
NAIBU WAZIRI WA WANAWAKE JINSIA NA WTOTO DKT PINDI CHANA AKIWASILI KATIKA CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI ULEMBWE
MKUU WA CHUO CHA ULEMBWE BWANA FRANCIS HAULE AKIWATEMBEZA WAGENI KATIKA MIRADI YA CHUO HICHO
SAMADI YA NG'OMBE AMBAYO TAYARI IMEKWISHA KUTUMIKA KATIKA MITAMBO YA BAYO GESI
JENERETA LA UMEME LINALOTUMIKA KWA SASA BAADA YA KUKOSEKANA KWA UMEME
MASHINE ZA CHELEHANI KWAAJILI YA UFUNDI USHONAJI
Naibu
waziri wa
wanawake Jinsia na Watoto Pindi Chana leo ameanza ziara ya siku mbili
mkoani Njombe kwa kutembelea vikundi vya Vikoba Makambako na vyuo vya
maendeleo ya jamii Ulembwe na Njombe mjini ambapo pamoja na mambo
mengine amewataka wananchi kuwapeleka watoto wao kujiunga ili kupata
elimu ya ufundi stadi ya kujitegemea Na kujipatia ajira kwa kujiajiri.
Akizungumza
akiwa katika chuo cha maendeleo Ulembwe Naibu waziri wa wanawake jinsia
na watoto Pindi Chana amewataka maafisa maendeleo kufanya kazi ya ziada
kwa kutembelea na kutambua changamoto mbalimbali zinazowakabili
wananchi ikiwemo vyuo vya ufundi stadi pamoja na kutoa elimu kwa jamii
kutambua umuhimu wa kujiunga na vyuo hivyo.
Aidha
Bi.Chana amepongeza kwa hatua za maendeleo zinazofanywa na wanachuo wa
Ulembwe kwa kutoa fani mbalimbali huku akichukua baadhi ya changamoto
ambazo zimekuwa zikivikabili vyuo vya maendeleo ya Ufundi stadi hapa nchini na kwenda kuzifanyia kazi ambapo amesema pamoja na changamoto
hizo vyuo hivyo vinatakiwa kubuni mbinu mbadala za kuweza kuwasaidia
kupunguza baadhi ya changamoto zilizo chini ya uwezo wao.
Mkuu
wa wilaya ya Njombe bi. Sarah Dumba pamoja na mambo mengine amemshukuru
waziri wa wanawake,jinsia na watoto kwa kuwatembelea na kusikiliza kero
zinazowakabili wanavyuo na vikundi vya akina mama na vituo vya watoto
na kwamba huenda ikawa mwafaka kwa mkoa wa Njombe kupelekewa misaada na
kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili.
KAIMU AFISA MAENDELEO YA JAMII WILAYA YA WANGING'OMBE MICHAEL HAULE
AKISOMA TAARIFA KWA MGENI RASMI MKUU WA CHUO FRANCIS HAULE
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH DUMBA AKIMKARIBISHA MGENI RASMI AMBAE NI
WAZIRI WA WANAWAKE JINSIA NA WATOTO NA MBUNGE WA VITI MAALUMU MKOA WA
NJOMBE
WAZIRI WANAWAKE JINSIA NA WATOTO PINDI CHANA AKITOA HOTUBA YAKE AKIWA KATIKA CHUO CHA MAENDELEO YA JAMII ULEMBWE
Naibu
waziri wa wanawake Jinsia na Watoto Pindi Chana leo ameanza ziara ya
siku mbili mkoani Njombe kwa kutembelea vikundi vya Vikoba Makambako na
vyuo vya maendeleo ya jamii Ulembwe na Njombe mjini ambapo pamoja na
mambo mengine amewataka wananchi kuwapeleka watoto wao kujiunga ili
kupata elimu ya ufundi stadi ya kujitegemea Na kujipatia ajira kwa
kujiajiri.
Akizungumza akiwa katika chuo cha maendeleo Ulembwe
Naibu waziri wa wanawake jinsia na watoto Pindi Chana amewataka maafisa
maendeleo kufanya kazi ya ziada kwa kutembelea na kutambua changamoto
mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwemo vyuo vya ufundi stadi pamoja
na kutoa elimu kwa jamii kutambua umuhimu wa kujiunga na vyuo hivyo.
Aidha
Bi.Chana amepongeza kwa hatua za maendeleo zinazofanywa na wanachuo wa
Ulembwe kwa kutoa fani mbalimbali huku akichukua baadhi ya changamoto
ambazo zimekuwa zikivikabili vyuo vya maendeleo ya Ufundi stadi hapa
nchini na kwenda kuzifanyia kazi ambapo amesema pamoja na changamoto
hizo vyuo hivyo vinatakiwa kubuni mbinu mbadala za kuweza kuwasaidia
kupunguza baadhi ya changamoto zilizo chini ya uwezo wao.
Mkuu wa
wilaya ya Njombe bi. Sarah Dumba pamoja na mambo mengine amemshukuru
waziri wa wanawake,jinsia na watoto kwa kuwatembelea na kusikiliza kero
zinazowakabili wanavyuo na vikundi vya akina mama na vituo vya watoto na
kwamba huenda ikawa mwafaka kwa mkoa wa Njombe kupelekewa misaada na
kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili.
Kwa upande wake
katibu wa chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe Hosea Mpagike amewapongeza
vijana na wazazi ambao wametambua umuhimu wa kujiunga na vyuo hivyo
ili kupatiwa elimu ya ufundi na kwamba hatua hiyo itasaidia kuwapatia
uwezo wa kujitegemea pindi watakapo kuwa uraiani kwa manufaa yao.
Awali
akisoma taarifa fupi kwa mgeni rasmi Mkuu wa chuo cha Maendeleo ya
wananchi Ulembwe bwana Francis Haule amesema kuwa pamoja na serikali
kuhamasisha vijana kujiunga na vyuo hivyo ili kujifunza ufundi stadi
lakini bado wananchi wanamuamko mdogo wa kupeleka watoto wao katika chuo
hicho ambapo mpaka sasa kina jumla ya
wanachuo hamsini na tatu huku bado kinauhitaji mkubwa wa wanafunzi wa masomo ya
ufundi.
Aidha bwana Haule amesema kuwa chuo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali
ikiwemo ukosefu wa miundombinu ya umeme,upungufu wa watumishi,ukosefu wa
usafiri,huku kikifanikiwa kutatua baadhi ya changamoto ikiwemo ujenzi wa
maabara,kujenga mtambo wa gesi ya samadi kwaajili ya kupikia pamoja na kutoa fani
mbalimbali za useremala,uashi,umeme wa nyumbani,ushonaji nguo,huku kikitoa masomo
ya stadi za maisha,hisabati,kiingereza,uchoraji, ujasiliamali na kompyuta.
Kwa upande wao wanafunzi wa chuo hicho wameshukuru uongozi wa chuo cha Maendeleo
cha wananchi Ulembwe kwa jitihada mbalimbali ambazo wamekuwa wakizifanya ili
kukabiliana na changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza huku wakipongeza mkuu wa
chuo kwani amekuwa msaada mkubwa kufanikisha maendeleo ya chuo hicho kwa kutafuta
wafadhili mbalimbali kusaidia chuo hicho.
Ziara hiyo ya Naibu waziri Wanawake ,Jinsia na watoto kesho inatarajia kuendelea katika
Wilaya ya Ludewa ambapo leo waziri huyo ametembelea kikundi cha wanawake UCLAS
makambako ambacho kinashughulika na mikopo ya wananchi vijijini VIKOBA ambapo
lengo la ziara hiyo ni kuwasikiliza wajasiliamali,vikundi na vyuo vya maendeleo na
changamoto zake.
KWA HISANI ya michaelngilangwa blogspot
No comments:
Post a Comment