Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Friday, May 30, 2014

ACHOMWA MOTO KWA WIZI WA NG'OMBE MKOANI MBEYA LEO ASUBUHI

 polisi kwa ushirikiano na wana nchi wakiuingiza mwili wa mwizi huyo kwenye gari ya polisi
 mzee akielezea kwa vyombo vya usalama 
ng'ombe aliye kuwa ameibiwa na mwizi uyo
WAKATI vyombo mbali mbali zikiendelea na jitihada za kuwaelimisha wananchi juu ya madhara ya kujichukulia sheria mkononi hali hiyo bado ni tete mkoani Mbeya.
 
Hali hiyo imezidi kujitokeza baada ya Wananchi wenye hasira kali wa Mwasanga Ivumwe jijini Mbeya kumpiga na kumchoma moto mwananchi mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja wakimtuhumu kwa Wizi wa Ng’ombe mmoja na ndama.
 
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo ameuambia mtandao huu kuwa tukio hilo lilitokea mapema leo asubuhi ambapo chanzo ni wizi wa Ng’ombe wa Kongoro Mwakitalima mkazi wa Isyesye kata ya Ilomba.
 
Alisema Ng’ombe huyo aliibiwa jana majira ya usiku ambapo mzee huyo alitoa taarifa kwa majirani ambao asubuhi walijihimu kutafuta ambapo walipofika maeneo ya  Ivumwe walikutana na mwendesha boda boda ambaye aliwaambia amekutana na mtu akiwa anaswaga hiyo mifugo.
 
Alisema baada ya kusikia hivyo waliamua kuanza kumfukuzia wakitumia bodaboda na ndipo walipofika eneo la Mwasanga relini walimkuta mtuhumiwa akiwa na hao Ng’ombe.
 
Alisema Wananchi mbali mbali walikusanyika na kuanza kumshushia kipigo kutokana na eneo hilo kukithiri kwa wizi wa mifugo lakini baada ya kipigo hicho mtuhumiwa alionekana kuwa ngangari jambo lililowatia hasira na kuamua kumchoma moto.
 
Shuhuda huyo aliendelea kusema baada ya kuanza kumchoma lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida mtu huyo hakuweza kukata roho hadi alipookolewa na Askari wa jeshi la polisi walipofika eneo la tukio.
 
Hadi tunaingia mtamboni hakuna taarifa zilizothibitisha kama mtuhumiwa huyo bado yuko hai ama amepoteza maisha.

No comments:

Post a Comment