
MASKINI Mungu wangu! Ndiyo maneno aliyoanza nayo kusema mama
mzazi wa mtoto Salome Abdallah Said (3), kutokana na mwanaye huyo afya yake
kuzidi kubadilika kufuatia kuumwa mara kwa mara licha ya kufanyiwa upasuaji
mara mbili.

Mtoto Salome Abdallah Said (3) akiwa na kovu tumboni baada
ya upasuaji.
Akizungumza na gazeti hili wiki iliyopita mama wa mtoto huyo
Veronica Laurent, mkazi wa Bunju B, jijini Dar es Salaam alisema kwamba mwanaye
kwa sasa hali yake siyo nzuri kwa vile amekuwa akijisaidia haja kubwa kupitia
mdomoni kama hapo awali, hali hiyo anasema ameambiwa na madaktari inasababishwa
na utumbo wake wa haja kubwa kujikunja.

HISTORIA YA MTOTO
Veronica anaeleza: “Mwanangu kwa sasa ana miaka mitatu, tangu nimzae katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar, aligundulika ana matatizo ya kutojisaidia haja kubwa kama kawaida ilibidi nipelekwe Hospitali ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.
Veronica anaeleza: “Mwanangu kwa sasa ana miaka mitatu, tangu nimzae katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar, aligundulika ana matatizo ya kutojisaidia haja kubwa kama kawaida ilibidi nipelekwe Hospitali ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.
“Nilimfikisha Muhimbili akiwa katika hali mbaya akawa anajisaidia haja kubwa kupitia mdomoni, hata hivyo, nikaambiwa tumpeleke Hospitali ya Agha Khan kwa vipimo zaidi, huko akagundulika kuwa utumbo wa haja kubwa umejikunja.”
AFANYIWA UPASUAJI MUHIMBILI
Katika maelezo yake mama huyo alisema kwamba mtoto wake
alifanyiwa upasuaji kwa mara ya kwanza tumboni na kuwekwa tundu ambalo alikuwa
akilitumia kutolea haja kubwa, baadaye akafanyiwa tena upasuaji kwa mara ya
pili chini ya tumbo na kuwekewa utumbo bandia lakini hata hivyo, ulikuwa
mwembamba hivyo ukawa haufanyi kazi vizuri.
UTUMBO WA BANDIA
“Tulipotoka Muhimbili na kurejea nyumbani haikuchukua siku
nyingi hali ya mtoto ikazidi kuwa mbaya, akawa analia kila mara nikaamua kurudi
Muhimbili.
“Madaktari baada ya uchunguzi wakasema utumbo wa bandia
aliowekewa ulikuwa mdogo na mwembamba hivyo ulishindwa kufanya kazi pia utumbo
ulikuwa umejikunja.
“Niliambiwa zinahitajika shilingi laki tisa ili afanyiwe
matibabu ambapo nimeshindwa kuzipata, bora awamu ya kwanza alijitokeza mdhamini
akatoa shilingi laki tisa. Nawaaomba Watanzania wenzangu wamsaidie mwanangu ili
kumnusuru na kifo, maana madaktari wamesema bila kufanyiwa hivyo anaweza
kupoteza maisha,” alisema mama huyo.
Akifafanua zaidi alisema: “Wakati fulani ili apitishe haja
kubwa katika njia ya kawaida inabidi ninunue dawa ya kulainisha kinyesi kwani
bila kufanya hivyo ni lazima ajisaidie kwa kupitia mdomoni.”
BABA YAKE ATOROKA
“Kwa sasa mtoto halali kutokana na kulia kutokana na maumivu
makali, baba yake baada ya kuona tatizo la huyu mwanangu alitoweka na kuzima
simu, hapatikani. Mimi nashindwa kufanya kazi yoyote.
Nawaomba Watanzania mnisaidie kupitia namba yangu ya simu
0712 004 677 au 0767 026 551,” alisema mama huyo huku akilengwalengwa na
machozi.
No comments:
Post a Comment