Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Tuesday, July 15, 2014

News:MOTO MKUBWA WAZUKA NA KUTEKETEZA MADUKA NA NYUMBA MWANANYAMALA JIJINI DAR ES SALAAMU


Duka la nguo likiwa linapamba moto na maduka mengine yakiwa yameanza kupamba moto pamoja na nyumba ambayo ilikuwa imeungana na duka.
 Moto ukiwa umeanza kama utani, watu wakiwa wanaendelea na kazi kama kawaida.
 Moshi ukiwa unazidi katika eneo ambalo maduka matatu yameteketea kwa moto.
Gari likiwa linarudi nyuma lilipotokea baada ya kuona kuna moshi mkubwa mbele yao.
 Mashuhuda wakiwa wameanza kuelekea eneo la tukio
 Moto ukiwa unaanza kupamba moto, waya wa umeme unao onekana unashuka chini ndio umesababisha moto huo.
 Moto ukiwa unazidi pamba moto katika duka la kushonea nguo na kuuza vitambaa.
 
 Mmoja ya vijana akiwa anaanza kuokoa vitu vyake jirani na maduka yaliyokuwa yakiungua.
 Moto ukiwa unazidi
 Mamia ya watu wakiwa wamefika kushuhudia  tutuki la Moto
 Kazi za uokoaji zikiwa zimeanza huku wasamalia wema wakisaidia kuhamisha vitu
 Maduka mengine yakiwa yameanza kushika moto kwa kasi
 Baadhi ya vyombo na vifaa vya duka la kushonea nguo vikiwa vimeokolewa
 Kazi ya uokoaji ikiwa inaendelea
 Mashuhuda wakiwa wanaongezeka.
 Moshi Mkubwa uliowachanganya watu na kila mmoja kuanza kutaka kukimbia eneo la tukio
Vijana wasamalia wema wakiwa wameacha kazi zao za kutengeneza magari, kufyatua matofari na mambo mengine wakiwa wanafanya kazi ya kuanza kuuzima moto.
 Vijana wakiwa wameanza kufanya kazi ya kuzima moto baada ya Kikosi cha zima moto kuendelea kuchelewa kufika
Maduka yakizidi kwisha kwa kuteketea kwa moto, Huku wananchi wakipata tukio moja kwa moja
 Baadhi ya Vijana wasamalia mwema wakiwa wanaondoa mabati ili kuzuia moto usiendelee kuwaka zaidi
Sehemu ya nyaya za umeme uliosababisha moto huo.
 Upande mwengine wa mashuhuda
 Vijana wakiwa bize wanafanya kazi ya kuendelea kuzima moto kwa ushirikiano
 Vijana wakiwa wanashughulika kwa nguvu zote ili wapate kuzima moto mara moja
 Baadhi ya Mashuhuda wakimwagiwa maji kupisha njia ya waokoaji waliojitolea kuzima moto kupita
 Mmoja wa Mashuhuda akiwa anachukua tukio kwa umakini
 Kikosi cha zima moto wakiwa wakiwa wanawasili eneo la tukio, huku wananchi wakiwazuia wasifanye kazi kwa kuwa kazi wamekuta imeisha
 Kikosi cha zima moto wakiwa wameanza shuguli ya kumalizia kuzima moto
Maji ya kuwasha yakiwa yamefunguliwa ili kuwatawanya watu wakae mbele kupisha kazi ya kuzima moto na uharifu.
 Kikosi maalum cha kuzuia vurugu cha Jeshi la Polisi (FFU) wakiwa  wamefika eneo la  tukio kwa ajili ya kulinda usalama
 TANESCO wakiwa wamefika eneo la tukio
Vijana wakiwa wanalalamikia kikosi cha kuzuia moto kuwa wamechelewa kuzima moto.
 Watu wakiwa wanazidi kuzuiliwa kupisha kazi ya uokoaji.
 Kikosi Maalum cha kuzuia vurugu kutoka Jeshi la Polisi FFU wakiwa wanaongezeka kuongeza kuvu ya kuimarisha ulinzi
 Kazi ya uokoaji ukiwa unaishia
 Kikosi maalum cha zima moto wakiwa wanamalizia kazi ya kuzima moto kidogo uliobakia
 Kila mtu anajitahidi kupata tukio
 Kazi ikiwa inaelekea kumalizika
 Baadhi ya mabaki uya mabati.
Kazi ya kuzima moto ikiwa imeisha , mmoja ya wanakikosi cha wazima moto akiwa anafunga mtambo
 Hivi ndivyo maduka yalivyobakia pamoja na nyumba iliyo ungua
 Mabaki ya vitu katika duka la vitambaa ya nguo na ushonaji
 Mmoja ya wanakikosi cha zimamoto akiwa anaongea na wananchi
 Wananchi wa mwananyamala wakiwa wanasikika wakisema "Wamekuja zima moshi... wamekuja zima moshi..."
 Mmoja wa wazee wa Mwananyamala aliye vaa shati la Dhambalau akiwa anakanusha kuwa ni uongo kwamba Kikosi cha kuzima moto hakijafanya kazi bali wananchi ndio waliozima moto
 Mmoja wa mashuhuda akiwa anaelezea jinsi moto ulivyotokea na kushukuru wananchi na Kikosi cha kuzima moto kwa kazi kubwa iliyofanikisha zoezi ka kuzima moto.
 Kazi ikiwa imeisha hizi ndizo ndoo ambazo zilisaidia kwa kiasi kikubwa kuzima moto pamoja na baadhi ya vijana wachache walio saidia kuzima moto huo.


*******

Moto mkubwa uliosababishwa na hitirafu ya umeme  zuka katika eneo la Mwananyamala Jirani na Hospitali ya Mwananyamala na kusababisha kuungua kwa Maduka matatu pamoja na nyumba moja ambayo ilikuwa imeungana na duka moja wapo ambalo walikuwa wanauza vitambaa na kushona nguo.
Moto huo ulichukua zaidi ya masaa mawili ambapo wakazi wa eneo hilo ndio waliosaidia kwa kiasi kikubwa kuzima moto huo mpaka kuumaliza na baadae Kikosi cha zima moto kufika na kukuta moto ndio unaishia na kuendelea kumalizia kushirikiana na wananchi wengine kuzima moto huo.
Katika tukio la Moto huo hakuna mtu ambaye amedhurika ingawa katika maduka yote matatu walifanikiwa kuokoa baadhi ya vitu huku vilivyobakia kuteketea vibaya kwa moto huo.

1 comment:

  1. Hi,am japanese woman.Some time read the this site. I studying swahili. Now Tanzania is change everyday. I hope everypeople get the more good LIFE!!

    ReplyDelete