Halima Mdee akianza kutoa chozi baada ya wanachama wa CHADEMA, kumchukulia fomu za kuwania nafasi ya Uenyekiti wa Taifa wa Baraza la Wanawake wa Chadema ( Bawacha)
Baadhi ya wanachama wa Chadema wakiwa nje ya ofisi za Bawacha walipofika kumchukulia fomu za kuwania nafasi ya Uenyekiti Mbunge wa Kawe, Halima Mdee.
Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Nadia Said akipokea fomu kutoka kwa Katibu Muhtasi wa Mabaraza, Neema Alex

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akipokea fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Wanawake wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha), kutoka kwa mwanacha wa Chadema tawi la Ununio, Nadia Said mara baada kundi la wanachama wa chama hicho kumchukulia fomu ili awanie nafasi hiyo.
Nipeni muda wa kwenda kutafakari jambo hili.... .alisema Halima. Hivi nitaweza kweli?

Halima Mdee akipongezwa na akinamama waliomkabidhi fomu.


Halima Mdee akiingia katika Ofisi cha Chadema huku akisindikizwa na wanachama wa chama hicho.
No comments:
Post a Comment