Wasamalia wema wakijaribu kuokoa maisha ya dada aliyegongwa na gari (daladala) maeneo ya Ubungo maji wakati akivuka barabara.
Mwanamke mmoja (jina halijafahamika) aliyekuwa anavuka barabara ya Morogoro maeneo ya Ubungo maji kutoka ng'ambo ya tank na kuelekea upande wa Tanesco amegongwa na gari ya daladala aina ya Toyota Coaster lililodaiwa kuvunja sheria likiwa linapita kwenye barabara ya magari ya mwendo kasi. Katika ajali hiyo dereva wa basi(daladala) hakupatikana kwani alikimbia baada ya ajali.

Majeruhi (dada huyo) akichukuliwa kwenye gari na wasamaria wema.

Mmoja wa mashuda wa ajali
ameiambia blog hii ya Pamoja kuwa mama huyo alipogongwa na daladala lá inayofanya
kazi zake kutoka Mbezi - Muhimbili alafu likamburuza yapata mita kumi na tano,
baada ya daladala kusimama yule mama akawa anajitahidi kutoka pale
uvunguni lakini ilishindikana na damu zilikuwa zinavuja kichwani.
Mpaka walipo shuka abiiria wote waliokuwa wamepanda daladala hiyo na kuliinua
na kumtoa mama huyo kwenye daladala ,na baada ya kutokea ajali hiyo dereva wa
daladala hiyo alikimbia.
No comments:
Post a Comment