Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Monday, September 22, 2014

AUAWA KWA KUCHOMWA KISU TUMBONI NA KUPORWA PIKIPIKI DODOMA

 Tukio hili limetokea eneo la Bonanza kata ya Chamwino, Dodoma mjini. Kwa shuhuda wetu aliyekuwa eneo la tukio  amesema kuwa dereva wa bodaboda amekutwa amefariki  baada ya kuuliwa na watu wasiojulikana  na kisha watu hao kutoweka  bodaboda aliyokuwa akiendesha marehemu huyo. Dereva huyo wa bodaboda  amechomwa kisu maeneo ya tumboni na shingoni katika mwili wake na katika eneo la tukio kumekutwa visu viwili amavyo vinasadikika kutumiwa katika uharifu huo kando kidogo ya barabara na sehemu ulipokuwa mwili wa marehemu.
 Hiki ni mojawapo ya kisu kinachosadikiwaa kutumika katika kufanya mauaji hayo ya dereva wa Bodaboda na kisha watu hao kutoweka na pikipiki.
 Damu ikiwa imetapakaa eneo la tukio
 Hii ni mojawapo ya sehemu aliyochomwa kisu dereva huyo wa bodaboda 
Baadhi ya mashuhuda wakiwa kwenye eneo la tukio

No comments:

Post a Comment