Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Wednesday, October 15, 2014

KIJANA AKUTWA AMEFARIKI KATIKA KORONGO LA LUBENGELA MKOANI KIGOMA

Polisi wakibeba mwili wa marehemu katika korongo hilo
Kutokana na eneo alilokutwa marehemu kuwa na miundombinu mibovu ya kumtoa walilazimika kutumia ngazi,hivyo waliomba msaaada wa ngazi kwa gari la 'emegency' la Tanesco na hapa ngazi ilikuwa inashushwa tayari kwa mwili wa marehemu kupandishwa juu kupelekwa eneo husika.
Katika hali ya kustajaabisha kijana mmoja alietambulika kwa jina moja la Yusuph (Me) mkazi wa Buzebazeba Ujiji amekutwa amefariki katika korongo la Lebengera jirani na Ofisi za CCM mkoa katika manispaa ya Kigoma Ujiji huku akiwa amejaa damu katika paji lake la uso

Mara baada ya Jeshi la Polis kufika eneo la tukio walimpekua marehemu na kumkuta na fedha taslimu kama elfu tatu hivi na karatasi ambayo haikujulikana maramoja imeandikwa nini
 tukio hilo limetokea Oktoba13 eneo tajwa hapo juu huku umati mkubwa ukiwa umefurika ili kumtambua na kushuhudia tukio hilo,

katika uchunguzi wa awali inasemekana tukio hilo limetokea usiku wa siku hiyo,kwani kutwa nzima ya siku hiyo hapakuonekana mtu ambae amekufa katika eneo hilo.

mmoja wa wananchi aliekuja kushuhudia tukio,na ambae ni mfanyakazi katika ofisi moja jirani na eneo la tukio( jina kapuni) amesema hii imekuwa ni mara ya pili kutokea tukio kama hili la mtu kukutwa ameuawa na kutupwa katika korongo hili,hivyo anaviomba vyombo vya usalama kuweka doria ya mara kwa mara eneo hili kwani eneo hili linakaribiana na Bar pamoja na Ofisi za Hazina Ndogo.

No comments:

Post a Comment