Halima Mdee na wenzake wakitoka mahakamani baada ya kuachiwa huru kwa dhamana leo.
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na wenzake 8 leo wamepata dhamana katika
Mahakama ya Kisutu, Dar. Kesi yao kutajwa tena Oktoba 21, 2014.
Siku ya jana washtakiwa hao walipanda kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi
Kaluyenda na kusomewa mashtaka mawili na Wakili wa Serikali Mkuu,
Kangola aliwataja washtakiwa kuwa ni Mbunge wa Kawe, Mdee, Rose Moshi,
Penina Peter, Anna Linjewile, Mwanne Kassim, Sophia Fanuel, Edward
Julius, Martha Mtiko na Beatus Mmari.
Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee akionesha ishara ya Chadema baada ya kuachiwa huru kwa dhamana leo.
Mdee na wenzake hao wanashitakiwa kwa makosa mawili la kwanza
washtakiwa wote wanadaiwa Oktoba 4 mwaka huu, Mtaa wa Ufipa wilayani
Kinondoni, walikaidi amri ya Ofisa wa Polisi SP Emmanuel Tillf
iliyowataka watawanyike.
Shtaka la pili washtakiwa wote wanadaiwa Oktoba, mwaka huu, maeneo ya
mtaa wa ufipa jijini Dar es Salaam wakiwa na lengo moja walikusanyika
kinyume na sheria wakitaka kwenda ofisi ya rais.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Wakili wa kujitegemea wa Chadema, Peter Kibatara, akizungumza na wanahabari.
Halima akiwa na wanachama wa Chadema baada ya kuachiwa huru.
Halima Mdee akisalimiana na wanachama wake baada ya kuachiwa huru.
Wafuasi wa Chadema wakijiandaa kuwapokea wanachama wao baada ya kuachiwa huru.
Wafuasi wa Chadema wakionyesha bango lenye ujumbe wa kumpongeza mbunge wao.
Mdee akiwa juu ya gari akitoka nje ya mahakama.
Gari la wanachama wa Chadema likitoka katika mahakama.
No comments:
Post a Comment