Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Thursday, October 30, 2014

WATU 12 WAPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI ILIYO TOKEA MKOANI ARUSHA JANA JION

Ajali imetokea jana jioni  katika eneo la Tengeru, Jijini Arusha ikihusisha gari dogo aina ya Toyota Hiace yenye namba za usajili T519 DBJ (pichani juu) inayofanya safari zake kati ya Usa River na Stand ya mabasi ya mkoani Arusha na Lori la Mafuta lenye  namba  za  usajili  T582 ACR. Chanzo cha Ajali hiyo inaelezwa kwamba ni hiyo daladala lilikuwa likijaribu kulipita gari jingine ndipo ilipokutana na lori hilo la mafuta na kugongana uso kwa uso na kusababisha vifo vya abiria kumi na mbili (12) waliokuwa ndani ya daladaa hiyo 
Watu 12  wamekufa papo hapo na wengine wawili kujeruhiwa baada ya basi  dogo aina ya Toyota Hiace maarufu kama kipanya walikokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori la mafuta.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo jana majira ya saa 10 katika  eneo  Makumira  wilayani  Arumeru.

Sabas, alisema  ajali  hiyo  ilitokea baada ya kipanya hicho aina ya Nissan T519 DBV kilichokuwa kikitokea  jijini  Arusha  kwenda  Usa River kuhama upande na kugongana uso kwa uso na  lori hilo  lenye  namba  za  usajili  T582 ACR lililokuwa  likitoka  Moshi mkoaniKilimanjaro kwenda Arusha Sabas alisema majeruhi wa ajali  hiyo   wamepelekwa  Hospitali  ya   Wilaya  ya  Tengeru kwa matibabu.

Alisema  miili ya marehemu hao   imehifadhiwa Hospitali  ya mkoa  wa Arusha ya Mount  Meru kusubiri ndugu kuichukua kwa maziko.

Alisema baada ya ajali  hiyo kutokea  dereva  wa  lori  hilo alikimbia   na kwamba polisi wanaendelea  kumtafuta.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya rufani ya Mount Meru, Dk. Josiah Mray, alithibitisha kwamba walipokea maiti za watu 12 waliokufa papo hapo katika eneo la ajali.Dk. Mray alisema kuwa walipokea majeruhi mmoja ambaye hali yake ni mbaya.

Hadi tunakwenda mitambo, Sabas hakutaja majina ya marehemu hao kwa kuwa zoezi   la   kuwatambua pamoja na majeruhi hao lilikuwa linaendelea na kuahidi kutoa taarifa baada ya kukamilika.

No comments:

Post a Comment