Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Wednesday, November 12, 2014

TANGAZO LA MSIBA WA NDUG.ROBERT VICTOR LENGEJU

Familia ya Lengeju wa Kipera Mkoani Morogoro wanasikitika kutanga kifo cha mdogo wao ROBERT VICTOR LENGEJU kilichotokea mchana wa leo katika Hospitali ya TMJ Dar es Salaam.

Mipango ya mazishi inafanyika Nyumbani kwa kaka yake Charles Lengeju, Njia panda Airport jijini Dar es Salaam.



Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki wote wa familia ya Lengeju na wakazi wa Kipera mkoani Morogoro. 

RATIBA YA KUAGA MWILI LEO NA MAZISHI YA ROBERT VICTOR LENGEJU
Familia ya Lengeju wa Kipera Mkoani Morogoro na Dar es Salaam inapenda kuwatangazia ndugu jamaa na marafiki wote wa marehemu ROBERT VICTOR LENGEJU na Familia ya LENGEJU kuwa kijana wao mpenda aliyefikwa na umauti Novemba 10, 2014 katika Hospitali ya TMJ baada ya kuugua kwa muda mfupi anataraji kuzikwa kesho Alhamisi nyumbani kwao Kijiji cha Kipera, Kata na Tarafa ya Mlali Wilayani Mvomero mkoa wa Morogoro.

Kipera ipo mbele kidogo ya Chuo Kikuu cha Mzumbe.

Mwili wa marehemu ROBERT LENGEJU, utaagwa leo kuanzaia saa 6:00 mchana baada ya Misa katika Kanisa Katoliki Msimbazi Dar es Salaam na baade jioni kusafirishwa hadi Morogoro.

Kesho Novemba 13 2014, kuanzia saa 5:00 Asubuhi taratibu za mazishi zitaanza nyumbani kwao KIPERA kwa misa takatifu na maziko.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.

No comments:

Post a Comment