Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Wednesday, January 7, 2015

NES ATHIBITISHA MTOTO ALIYE ZALIWAKUFARIKI WAAKATI YUKO HAI

mama mmoja mjamzito alikwenda Hospitali ya Mkoa Morogoro siku ya jana, alipofika hospitali hapo hakupata huduma nzuri kutoka kwa nesi aliyekuwa zamu, baada ya uchungu kumshika alihangaika bila msaada wowote na mwisho wake akajifungua chini.
 
Wakati huo ilikuwa usiku, umeme ulikuwa umekatika na wakalazimika kutumia tochi ya kwenye simu wakati akijifungua.

Nesi huyo alikuja kumpa msaada baadaye akamwambia kwamba tayari mtoto wake ameshafariki, hivyo awaite ndugu zake ili wamchukue mtoto huyo wakazike.

Ndugu walimchukua mtoto huyo akiwa amewekwa ndani ya  ndoo, walipofika nyumbani waligundua kwamba mtoto alikuwa mzima bado lakini waliporudi tena Hospitali jitihada za kumtibu hazikusaidia kwani alifariki wakati wakianza jitihada za kumshughulikia.


Mganga Mkuu Hospitali ya Mkoa Morogoro amesema kuwa hakuwepo kwa kuwa yupo likizo.

No comments:

Post a Comment