Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Tuesday, March 10, 2015

MBUNGE WA KIGOMA KASKAZINI ZITTO KABWE AVULIWA UWANACHAMA KATIKA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

 Mnadhimu Mkuu Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, akitoa tamko la kumvua uanachama Zitto Zuberi Kabwe leo.
 Waandishi wa habari wakifuatilia tukio hilo.

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini,  Zuberi Zitto Kabwe, amevuliwa uanachama wake mchana huu katika ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jijini Dar es Salaam katika hatua iliyotangazwa na mnadhimu mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu, baada ya mbunge huyo kushindwa kesi iliyokuwa amefungua katika Mahakama Kuu ya Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi hizo, Lissu alisema Zitto amefutwa uanachama  kwa mujibu wa taratibu na sheria ya chama isemayo  kwamba endapo mwanachama atapata tatizo lolote binafsi ama la kichama, malalamiko yote yatasuluhishwa ndani ya chama na si mahakamani
“Hivyo,  kwa mujibu wa sheria za chama, Zitto alikiuka sheria  anapaswa kuvuliwa uanachama wake,” alisema Lissu.

Lissu aliongeza kuwa hata kama Zitto angeweza kwenda kushitaki lazima angeanzia katika mahakama ndogo za wilaya yaani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi au Masijala ya Mahakama ya Wilaya  tofauti na alivyopeleka kesi hiyo moja kwa moja Mahakama Kuu.
Mahakama hiyo pia imemtaka mbunge huyo wa zamani kukilipa chama hicho gharama zote za kesi hiyo kama ilivyoelekezwa na mahakama, na kwa mujibu wa Lissu,  Chadema kitakaa na kutathmini gharama husika.
Kuhusu utambulisho wa Zitto bungeni, Lissu alisema  kwa mujibu wa kanuni za chama chake, katibu wa chama chake anatakiwa kumwandikia barua Mwenyekiti au Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi kumjulisha  Zitto tena si mwanachama wao na taratibu zingine zitafuatia
Chanzo:GPL

No comments:

Post a Comment