Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Friday, May 1, 2015

18 WANUSURIKA KATIKA AJALI YA BASI ILIYOTOKEA MKOANI IRINGA LEO

Baadhi ya  wananchi  wa  mjini Iringa na abiria  wa basi la Embakasy  wakitazama basi hilo  lililopinduka leo eneo la Ipogolo mjini Iringa . 
Abiria wakiwa wanatzama ajali hiyo mara baada ya kunusurika katika basi walilokuwa wakisafiria
wasamalia wema wakiwa wanasaidia kutoa mizigo iliyokuwepo katika basi 

AJALI yanua mmoja  Iringa huku abiria  18  wakinusurika   kifo baada ya  basi  la kampuni ya  Embakasy  lenye namba  za  usajili  T 997 AKJ kuacha  njia ya  kupinduka  eneo la Ipogolo  mjini Iringa.

Wakizungumza na mtandao huu   eneo la  ajali  baadhi ya abiria  wa  basi hilo  walidai  kuwa basi  hilo  lilikuwa  likitaka kuingia katika  kituo  kimoja  wapo  cha  mafuta eneo hilo  na  wakati  likitoka  ndipo  liliponusurika  kugongana na lori  lililokuwa barabara  kuu ya Iringa - Mbeya   .

Hivyo  kutokana na kunusuri kugongana ndipo  dereva wa  basi hilo alipoamua  kulikwepa lori  hilo kwa  kukata  kuna kubwa  zaidi  iliyopelekea  basi hilo  kuacha  njia na  kupinduka kando ya  barabara  hiyo .

Walisema  kuwa  basi  hilo  limekuwa  likifanya  safari  zake kati ya Ilandutwa wilaya ya  Iringa vijijini na Iringa mjini na  kuwa pona  yao katika ajali  hiyo ni  kutokana na kuwa katika  mwendo  wa kawaida  zaidi .

konda  wa  basi hilo  Bw  Esack  Mtandi  alielezea  tukio  hilo  alisema  kuwa  basi   hilo  lilikuwa  likitaka  kuingia kujaza mafuta  katika  kituo  kimoja wapo cha  mafuta kilichopo  eneo  hilo na  mbele  kulikuwa na  lori  na  wakati   dereva  akijiandaa  kuingia  kituoni  hapo  ghafla usukani  uligoma na  hivyo  kumtoa  dereva  nje ya barabara kabla ya  kupinduka .

Alisema  katika basi  hilo kati ya abiria  18  waliokuwepo  abiria  6  ndio  waliojeruhiwa akiwemo  dereva na  hakuna  aliyepoteza masisha .

Kwa  upande  wake  jeshi la  polisi  mkoani Iringa  limethibitisha  kutokea kwa ajali hiyo na  kuwa  ajali   hiyo  ilitokea majira  ya saa 3  kasoro asubuhi ya  leo   na  kumtaja  dereva  wa  basi hilo  kuwa ni Abdalah Nyalusi 

Alisema  kamanda  wa  polisi  mkoa  wa  Iringa Ramadhan  Mungi na  kuwa katika  ajali  hiyo  hakuna abiria  aliyepoteza maisha .
 
Wakati  huo  huo mmoja kati ya  wafanyabiashara  maarufu mji  wa Ilula   wilayani  Kilolo  mkoani hapa  aliyefahakika  kwa jina  moja la kasim aliyekuwa  akiendesha gari  lenye namba za  usajili T 111 GRE RAV4 amekufa  papo  hapo baada  ya kugongana  uso  kwa  uso la lori .

Kamanda  Mungi  alisema  kuwa mfanyabiashara   huyo  alikuwa  akitokea  Ilula  kuja  Iringa  mjini na baada ta  kufika  eneo la kona  ya Igumbilo  barabara  kuu ya  Iringa - Dar es salaam  wakati  akijaribu kulipita daladala  lililokuwa mbele yake  katika  kona    hiyo ghafla  alikutana na lori  hilo na kugongana  nalo .

Hata  hivyo  alisema  jina kamili  la mtu  huyo bado  kufahamika na  kuwa  wanasubiri  ndugu zake  ili  kujakutambua mwili  huo na  kutoa  jina kamili.

1 comment: