Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Saturday, May 9, 2015

KAMPUNI YA DAR EXPRESS YAPOTEZA BASI LAKE LILILO TEKETEA KWA MOTO LEO KATIKA BARABARA YA ARUSHA,CHALINZE ENEO LA MAKOCHO

 Taarifa zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani SACP Jafari Ibrahimu kwamba basi la kampuni ya Dar Express limeteketea kwa moto likiwa safarini kutokea Dar es salaam kuelekea Arusha likiwa abiria wa kutosha kama ilivyo abiria wanavyokuwa wamejaa kwenye mabasi.


Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani anasema 
‘Ni kweli basi la Dar Express leo saa saba mchana limeteketea kwa moto katika kijiji cha Makocho kijiji hiki kiko katikati ya kijiji cha Mandera na Mbwewe ndani ya Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani lilipata hitilafu likaanza kuungua lenyewe, bahati nzuri abiria wote wamewahi kushuka salama ila basi limeteketea lote, hawakuwahi kulizima na hakuna aliejeruhiwa

No comments:

Post a Comment