Wananchi wakiangalia ajali ya gari ambalo ni daladala lenye namba za usajili T 456 BVT lililoacha njia kutokana na mwendokasi na kuparamia genge pamoja na bajaj yenye namba MC 611 ADC, maeneo ya Kitunda relini barabara ya Mombasa kwenda Moshi Baa Dar es Salaam leo asubuhi. Imeelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa daladala kukimbilia abiria. Katika ajali hiyo hakuna mtu aliyejeruhiwa.
Gari(Daladala) hiyo likiwa ndani ya genge baada ya kuacha njia.
Bajaj namba MC 611 ADC, likiwa kando ya daladala hiyo baada ya kugongwa.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)
No comments:
Post a Comment