Kuishiwa nguvu za kiume ni jambo la kawaida kwa wanaume wengi
hasa wenye umri mkubwa. Hatari ya kupungukiwa nguvu za kiume huongezeka
kutokana na umri. Kulingana na tafiti za kitabibu, wanaume wenye umri
kuanzia miaka 60 tatizo hili ni kubwa kwao kuliko wanaume wenye umri wa
miaka 40.
Wanaume wenye elimu ndogo juu ya utendaji kazi wa mwili na afya ndiyo
wanaokabiliwa sana na tatizo hili. Hii ni kwa sababu wanashindwa
kuelewa aina ya chakula kinachoongeza nguvu za kiume na za mwili kwa
ujumla, mtindo wa maisha wanayotakiwa kuishi ili kupunguza hatari hiyo,
wanakunywa pombe na hawafanyi mazoezi ya viungo.
Mazoezi ya mwili hupunguza hatari ya kupungukiwa nguvu za kiume.
Tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume linaweza kuwa na sababu za kihisia
(emotional causes) lakini sababu nyingine hutokana na maradhi kama vile
kisukari na shinikizo la juu la damu. Inakadiriwa kuwa asilimia 50 hadi
60 ya wanaume wenye maradhi ya kisukari wana tatizo hili.
Watu wanaosumbuliwa na kiharusi na ulevi nao wana hatari kubwa sana
kwa sababu ya uharibifu wa korodani yaani testicles kutokana na ulevi
sugu na kupoteza testerone. Pombe hupunguza kwa kiasi kikubwa uzalishaji
wa manii au mbegu za kiume.
Watu wanaosumbuliwa na shinikizo la damu, magonjwa ya tezi, majeraha
kama vile kutokana na upasuaji wa viungo vya uzazi, matumizi ya dawa
zenye kemikali bila mpangilio au ushauri wa wataalamu na maradhi ambayo
hudhoofisha mtiririko wa damu kwenye uume. Hata hivyo, upungufu wa nguvu
za kiume unatibika katika umri wa rika zote.
Vipengele ambavyo daktari atahitaji kuvifahamu kabla ya kuanza
kukutibu tatizo la kuishiwa nguzu za kiume ni;Umri wa mgonjwa, jumla ya
afya aliyonayo kwa sasa, utendaji wa tendo la ndoa zamani na sasa,
migogoro ya ndoa, kifamilia, kazi nk.
TIBA Ni muhimu wewe kujisikia vizuri na kumwamini daktari wako,
kisaikolojia utakuwa umepiga hatua ya kwanza ya kupata nafuu ya tatizo
linalokukabili, nenda akakupime na anaweza kukupa dawa kama ataona
inafaa. Kwa ushauri wa bure piga au tuma ujumbe namba zilizopo hapo juu.
No comments:
Post a Comment