Kassu Ent iliandaa tamasha
maalum kutoka kwa wasanii wetu wa kizazi kipya iliowajumuisha Barbaba na
Suma Lee. Tamasha hili lilikwenda sambamba kwa kusherekea miaka 51 ya
Uhuru wa Tanzania Bara iliyofanyika siku ya jumamosi tarehe 22.12.12
jijini London katika ukumbi wa Stratford.
Mgeni rasmi alikua naibu
Balozi Chabaka Kilumanga alieambatana na mkewe Irene Kilumanga. Aidha Mh
Balozi Kilumanga aliwapongeza watanzania walioweza kuja kujumuika na
kusherekea pamoja katika siku hii na kuwasihi kuendeleza mshikamano kwa
kuishi pamoja kwa amani na upendo.
Kwa maelezo zaidi picha na tarehe za shoo zijazo tembelea www.jestina-george. com
Taarifa imetumwa na Frank Eyembe wa Urban Pulse.
No comments:
Post a Comment