Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Monday, October 14, 2013

PICHA ZA VURUGU ZA WANANCHI MOROGORO...NYUMBA ZACHOMWA, GARI LA MKURUGENZI LAHARIBIWA....TAZAMA HAPA

Vurugu za wakulima zimezuka tena Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro ,ambapo kundi la wakulima limefunga barabra ya Turiani-Morogoro eneo la Mkindo wakipinga wafungaji kuchoma nyumba kadhaa za wakulima sambamba na kushinikiza serikali kuwaruhusu kulima kwenye bonde la Mgongolwa.

 
 Gari la mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero likiwa nje ya kituo cha polisi Dakawa.


Katika vurugu hizo wakulima hao walirusha mawawe yaliyosababisha Polisi mmoja kukimbizwa hospital baada ya kupigwa jiwe kwenye paji la uso huku gari la mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mvomero likihalibika vibaya baada kupigwa mawe na wakulima hao.



Askari wa jeshi la Polisi akikagua gari la mkurugenzi lililoaribiwa vibaya katika vurugu hizo.

waandishi wa habari wa waliofika eneo la tukio pia walipigwa mawe na wakulima hao na kushindwa kutekeleza majukumu yao na kuamu kuondoka eneo hilo la tukio.Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Bw Anthony Mtaka alilaani kitendo kilichofanywa na wakulima hao na kulipongeza jeshi la polisi kwa kutumia hekima kwenye vulugu hizo licha ya kupigwa mawe na wakulima hao





Kundi la polisi wa kutuliza ghasi kutoka moorogoro mjini likieleka eneo la tukio 


No comments:

Post a Comment