Makazi mapya baada ya nyumba zao kuchomwa moto
Watoto: Wanacheza hawajui kinachoendelea
Ni majonzi makubwa
Hizi ndizo nyumba zao , wanalala chini ya miti baada ya nyumba zao kuchomwa moto
Wakazi wa kijiji cha kabage wakihama kijiji hicho baada ya nyumba
zao kuchomwa na askari waliokuwa wanafanya oparesheni ya kuwasaka
majangili nyumba hizo zilichomwa wiki iliyopita kijijini hapo na
kusababisha maelfu ya wanakijiji kuishi chini ya miti
Wakina mama wakiwa wanafungasha
Wakubwa kwa watoto wakiwa wanakihama kijiji hicho
Wakiendelea kuhama kijijini hapo
Wakazi wa kijiji cha Kabage wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi wakiwa
wanaishi chini ya miti na familia zao baada ya nyumba zao kuchomwa moto
na askari waliokuwa wanafanya oparesheni majangiri wiki iliyopita jumla
ya zaidi ya kaya 500 zilichomewa nyumba kijijini hapo na kuleta
malalamiko ya wanakijiji hao kwa kile wanachodai kijiji hicho ni halali
na kimesajiliwa kisheria toka mwaka jana na kupewa usajili wenye namba
KT/KIJ/47
Hawana makazi tena hawa
Mtoto akiwa amelala huku akiwa hana pa kuhifadhiwa ikiwa nyumba yao imechomwa moto
Mchungaji wa kanisa la PAG wa kijiji cha Mwamkulu Petro Mahenga
akimfariji mmoja wa wahanga waliochomewa nyumba zao katika kijiji cha
kabage wilayani Mpanda Daudi Belehiwa ambae pia mke wake aitwae Kurwa
Elias alijifungua mtoto ambae hajatimiza miezi yake kutokana na kutembea
kwa muda mrefu wakati akiwakimbia askari hao hata hivyo mtoto huyo
aliezaliwa akiwa na miezi nane alifariki muda mfupi baada ya kuzaliwa.
Vyombo vikiwa havina pa kupelekwa
Dogo akiwa ameishiwa Nguvu
Inasikitisha sana Wanakijiji hawa hawana makazi sasa
Na Walter Mguluchuma-Kativi yetu
Mpanda
Askari
waliokuwa kwenye operesheni ya kuwasaka majangili (iliyositishwa hivi
karibuni) waliokuwa wakiongozwa na JWTZ wamechoma moto nyumba za
wanakijiji cha Kabage Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi na kuwasababishia
wananchi hao kuishi chini ya miti na akina mama kujifungua kabla ya
wakati
Mwenyekiti wa
Kijiji hicho Maganga Kasope alisema tukio hilo lilitokea hapo Oktoba 28
mwaka huu majira ya saa tano asubuhi na kusababisha zaidi ya kaya mia
sita kukosa makazi ya kuishi
Alisema
kijiji hicho chenye wakazi zaidi ya elfu kumi ni kijiji halali kwani
kalisajiliwa toka mwaka jana na kupewa usajiri wenye namba za usajiri
wa kijiji KT/KIJ/47 hivyo wameshangazwa na wakazi wa kijiji hicho
kuchomewa nyumba zao wakati ni kijiji halali
alisema
kuwa katika tukio hilo akina mama watatu ambao walikua wajawazito
walilazimika kujifungulia kwenye mbuga za mpunga wakati wakikimbia
kuelekea kijiji cha jirani cha mwamkulu kujihifadhi hivyo kutokana
kutembea kwa umbali mrefu hivyo ililazimika kujifungulia njiani na
kujifungua watoto wakiwa salama
Kwa
upande wake mhanga wa tukio hilo Daudi Lulehiwa 28 alisema kutokana
na tukio hilo iliwalazimu ketembea umbali mrefu kwa ajiri ya kukimbilia
katika kijiji cha jirani cha Mwamkulu huku wakiwa wamebeba mizigo yao
na iliwalaziri hata watoto wao wadogo kutembea kwa miguu umbali huo
mrefu
Alisema
mkewe aitwaye Kulwa Elias 24 ambae alikuwa ni mjamzito wa miezi minane
kutokana na kutembea umbali huu huku akiwa amebeba mizigo aliweza
kujifungua mtoto wa wakike ambae alikuwa sio ridhiki na alifariki muda
mfupi baada ya kujifungulia chini ya mti
Nae
mchungaji wa Kanisa la wa Kanisa la P.A.G wa Kijiji cha Mwamkulu
Mchungaji Petro Mahega alisema toka wahanga hao waliokimbilia kijijini
hapo wamekuwa wakiishi kama wanyama wao na familia zao
Alieleza
kutokana na wahanga hao kuishi chini ya miti na mbaya zaidi hapo juzi
walinyeshewa na mvua ambayo ilinyesha majira ya usiku hivyo ametowa
jengo la Kanisa lake igawa ni dogo sana litumike kwa ajiri ya
kuwahifadhi wahanga hao
Kwa
upande wake mhanga mwingine Malidadi Gwachele 72 ambae anaishi na
familia yake ya watu 20 wakiwa chini ya mtu alieleza kuwa wameanza
kuhathirika kwa kupata magonjwa ya kuharisha
Alisema
hari hiyo imesababishwa na maji wanayo kunywa na mazingira wanayoishi na
hasa watoto wadogo ndio wanao athirika zaidi za magonjwa hayo
Mdae
Masanja alisema mbali ya kuchomewa nyumba yake pia amepoteza chakula
chake ambacho kiliteketea kwa moto baada ya kushindwa kukihamisha kwenye
nyumba yake wakati ikiungua
Alisema
sasa hivi wanalala nje bila hata kujali jinsia za familia walizo nazo
kutokana natukio lenyewe inawalazimu walale hivyo na wamekuwa
wakijisaidia kwenye vichaka
Aidha
Mhanga Katali Ngeleja alieleza mbele ya mwandishi wa habari hizi ambae
alitembelea eneo hilo kuwa wako watoto wenye umri kati ya miaka saba na
nane walipotezana na familia zao kwa muda wa siku mbili
Alieleza
yupo pia mwenzao mmoja ambae alikuwa anamiliki mashine ya kusanga unga
iliteketea kabisa kwa moto ikiwa ndani ya kibanda cha nyumba
No comments:
Post a Comment