Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Friday, November 15, 2013

BAADA YA MBEYA WAFANYABIASHARA KUSUSIA KUTUMIA MASHINE ZA TRA SASA MOROGORO KAZI IPO..

 Wafanya biashara wa Mkoa wa Morogoro wakiwa wamekusanyika wakijadili jambo.
Wafanyabiashara wa Mkoa wa Morogoro wamegoma kufungua maduka leo wakitaka kuonana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwa Lengo la kushinikiza kukataa mashine za kieletroniki za mamlaka ya mapato tanzania.Wafanya biashara hao wamegoma kufungua maduka tangu asubuhi wakishinikiza kuonana na mkuu wa mkoa jambo ambalo Mkuu wa mkoa amekubali na kuwaomba wateuliwe wawakilishi 8 kwa ajili ya kwenda kuonana naoa.Baada ya wawakilishi kuteuliwa bado wafanyabiashara hao walishinikiza kuandamana mpaka nje ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa ndipo Jeshi la Polisi walipoingila kati .

Jeshi la Polisi wakiwa katika barabara inayoelekea Kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Kulinda Amani na kuzuia maandamano yaliofanywa na wafanyabiashara hao.

Baadhi ya maduka yakiwa yamefungwa  Mjini  Morogoro  
 Wafanyabishara hao wakiandamana kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwa lengo la kushinikiza kuondolewa kwa mashine za Kieletroniki kwa madai kwamba ni kikwazo kikubwa katika biashara zao
 jeshi la polis likiwa limejipanga ili kulinda amani

No comments:

Post a Comment