Ilikuwa ni mida ya saa nane mchana ambapo Pantoni kubwa ya Mv. Magogoni ikiwa imesheheni abiria ikiwavusha kutokea Posta kuelekea Kigamboni , ilipatwa na wakati mgumu baada ya kushindwa kutia nanga ili iweze kusimama na abiria waweze kushuka..
Tukio hilo ambalo chanzo chake kimetokana na Injini za Pantoni hilo kushindwa kufanya kazi haikuweza kutia nanga kwa muda wote huo.. na ambapo kulikuwa na upepo mkali sana ambao ulisababisha Pantoni hiyo kukosa muelekeo na kuanza kuambaa ambaa mpaka maeneo ya Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere kisha kusukumwa zaidi hadi eneo la bandari ya Zanzibar.
Hata hivyo baada ya hali kuzidikuwa si nzuri walilazimika kuita meli ndogo za uokoaji ambapo meli ya kwanza haikuweza kuvuta pantoni hiyo na kulazimika kuongeza meli nyingine ili iweze kuongeza nguvu pamoja na boti za Jeshi la polisi ambazo zote zilifika na kwa ushirikiano mkubwa ziliweza kufanikiwa zoezi hilo la kuirudisha pantoni hiyo katika eneo lake husika.

Na abiria ambao walinusurika kuweza kushuka na kuendelea na shughuli zao za kawaida..

Baadhi ya Abiria katika Pantoni ya Mv. Magogoni wakiwa katika mshangao jinsi kivuko hicho kinavyo pepea pepea
Abiria wakiwa wamevaa mavazi maalumu ya kujiokoa na kujiweka sawa kama kungetokea hatari yoyote
wasafiri wakiwa wamejiandaa kwa kuvaa life jacket kwaajiri ya usalama zaidi
Wasafiri wakiwa na hofu ndani ya pantoni
baadhi ya abiria wakionekana kuwa na hofu
kutokana na pantoni hilo kupoteza muelekeo
kutokana na pantoni hilo kupoteza muelekeo
Ilikuwa ni baada ya kuanza kuvutwa na Meli zengine kuelekea katika eneo la kushukia, ambapo kila mtu alikua anaonekana mwenye nyuso ya furaha kuashiria kuokoka katika hatari.
Pantoni ya Mv. Magogoni ikiwa imetulia sasa na abiria wakiwa wanajiandaa kushuka.
Picha zote na Dar es salaam yetu Blog

No comments:
Post a Comment