Alitoa wito kwa mtu yeyote anayefahamu taarifa za mtuhumiwa huyo azitoe polisi ili aweze kukamatwa.
Katika
tukio la pili, mwanafunzi wa Shule ya Msingi Chekechea Ilongo, Onesmo
Haule (6), Mkazi wa Mahenje, amefariki dunia baada ya kugongwa na gari
lenye namba T.597 BGU, aina ya Toyota Coaster, iliyokuwa ikiendeshwa na Stanley Elia (44).
Kamanda
Msangi alisema, tukio hilo limetokea Machi 22 mwaka huu, katika
Kitongoji cha Ilongo, Wilaya ya Mbarali ambapo chanzo cha ajali hiyo ni
mwendo kasi wa dereva ambaye amekamatwa.
Katika tukio lingine, mwanafunzi wa darasa la tatu Shule ya Msingi Kiwira, iliyopo Wilayani
Rungwe,
Eva Mathias (11), mkazi wa Kijiji cha Ibiliro, amefariki dunia baada ya
kusombwa na maji ya Mto Kiwira alipoteleza katika daraja lililojengwa
kienyeji.
Kamanda Msangi alisema, tukio hilo limetokea Machi 20 mwaka huu, saa tatu asubuhi wakati marehemu akiwa na dada yake aitwaye Vero Lucas (20), ambaye baada ya tukio alitoa taarifa na ndipo juhudi za kumtafuta zilipoanza.
Chanzo;Majira
No comments:
Post a Comment