
Gurumo.
Mwanamuziki mkongwe pengine kuliko wote kwa sasa nchini na
mwasisi wa Bendi ya Msondo Ngoma, Muhidin Maalim Gurumo amefariki dunia
jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), alipokuwa akipatiwa
matibabu ya moyo.
Akizungumza jana mtoto wa kwanza wa marehemu
Abdallah Muhidin alisema baba yake alizidiwa juzi na kupelekwa Muhimbili
ambako aliendelea na matibabu hadi mauti yalipomkuta jana mchana.
“Alianza kuugua wiki tatu zilizopita, mwishoni
hali ilianza kubadilika akawa kila akila chakula anatapika. Hali yake
ilianza kubadilika, alipelekwa Muhimbili kwa matibabu,” alisema.
Alisema muda mrefu marehemu alikuwa akisumbuliwa
na tatizo la mapafu, shinikizo la damu na moyo. Marehemu ameacha mjane
na watoto sita.
Abdallah alisema marehemu atazikwa leo Masaki, Kisarawe na ataagwa leo adhuhuri nyumbani kwake Mabibo External, Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania
(Chamudata), Kassim Mapili alisema chama chake kimempoteza kiongozi wake
kwani hadi kifo chake, Gurumo alikuwa Mkuu wa Idara ya Fedha.
Desemba 14 mwaka jana wanamuziki wa dansi
wakishirikiana na wanamuziki wa kizazi kipya, walishiriki pamoja katika
tamasha la kumuaga nguli huyo baada ya kutangaza rasmi kustaafu muziki
akiwa amedumu kwa miaka 53. Hadi kustaafu kwake, Gurumo alizitumikia pia
bendi za Kilimanjaro Chacha, Rufiji Jazz, Kilwa Jazz, Sikinde na OSS.
Pia alikuwa kiongozi na mmoja wa wamiliki wa
Msondo Ngoma ambayo hapo awali ilijulikana kwa majina ya Nuta, Juwata na
Ottu. Gurumo ameitumikia Bendi ya Msondo katika majina yote ya nyuma
No comments:
Post a Comment