Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Monday, April 21, 2014

MOTO WAZUKA WATEKETEZA MADUKA MATATU NA MGAHAWA DODOMA USIKU WA KUAMKIA LEO


Wananchi wa mji wa Dodoma wakiangalia sehemu ya madhara ya tukio la moto uliotokea usiku wa kuamkia leo katika baadhi ya maduka yaliopo kwenye Barabara ya Nyerere Karibu na Makao makuu ya CCM mjini Dodoma,moto huo umeteketeza maduka matatu na mgahawa wa New Chick Villa Reustaurant. Maduka yaliyoathirika na moto huo ni Gulio La Mahafa Duka lililokuwa linauza bidhaa mbali mbali kwa jumla na reja reja zikiwamo bidhaa za Bakhresa,Duka la Esheki Investment lililo kuwa likiuza bidhaa za maofisini,vitabu na huduma ya uchapaji pomoja na Duka la madawa la lijulikanalo kama Kavula Pharmacy.Picha na Deusdedit Moshi,Globu ya Jamii Dodoma.

Wakazi wa Mji wa Dodoma wakiendelea kuangalia maduka hayo huku wengi wao wakiwa hawaamini kilichotokea.
Kila aliekatiza katika eneo hilo akusita kusimama na kuangaria athari hiyo ya moto kwenye Maduka hayo.
Sehemu iliyokuwa na maduka ikiwa imeteketea kabisa kwa moto uliotokea leo Barabara ya Nyerere karibu na Ofisi za makao makuu ya Chama cha Mapinduzi CCM.
Waokoaji wakihesabu baadhi ya bidhaa walizookoa kutoka stoo ya Magava Gulio. 
CHANZO :michizi blog

No comments:

Post a Comment