Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Thursday, June 19, 2014

NEWS ROUD;;WAWILI WAFARIKI KATIKA AJALI YA NEW FORCE,MKUU WA MKOA AFIKA KUSHUHUDIA AJALI HIYO HABARI NZIMA

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akiwa katika eneo la Ajali Jana 

Muonekano wa  basi la New Force Mbele Baada ya kupata ajali
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abass Kandoro akiwa anatembelea eneo la ajali hiyo ilipotokea
 Askari wa Usalama wa barabarani wakiwa eneo la tukio
 Basi la New Force upande 
 Miili ya watu wawili waliofariki katika ajali hiyo

 Kazi ya kuwaokoa abiria walioko ndani ya basi la New Force ikiwa inaendelea 
 Baadhi ya abiria wakiwa wameokolewa
Mmoja wa Majeruhi
Baadhi ya Mashuhuda wakiwa eneo la tukio
 Basi la New Force
 Mmoja wa Mashuhuda akilia kwa uchungu

Picha na David Nyembe

Mbeya yetu
WATEMBEA KWA MIGUU WAWILI WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA YA 1. THERESIA HINGI (65) NA 2. MARY KIZITO (26) WOTE WAKAZI WA IGURUSI WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA BASI LA KAMPUNI YA USAFIRISHAJI – NEW FORCE LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 952 CGU AINA YA SCANIA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA YAHAYA ABDALAH (39) MKAZI WA DSM.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 18.06.2014 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI KATIKA KIJIJI CHA IGURUSI, KATA YA IGURUSI, TARAFA YA ILONGO, BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA BASI HILO LILILOKUWA LIKITOKEA DSM KUELEKEA MBEYA MJINI LILIGONGA GARI T. 954 AMH AINA YA  FUSO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA TUPA ANYOSISYE (32) MKAZI WA KIWIRA –TUKUYU, KISHA KUACHA NJIA NA KUWAGONGA WATEMBEA.

AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU WENGINE WANNE WALIJERUHIWA KATI YAO ABIRIA MWANAUME MMOJA NA WANAWAKE WATATU WATEMBEA KWA MIGUU WOTE WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA MISHENI CHIMALA. PIA MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA DEREVA WA BASI, AMBAYE AMEKIMBIA MARA BAADA YA AJALI NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.  



KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA ALAMA NA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.

No comments:

Post a Comment