Baadhi ya
wacheza ngoma wa kikundi cha Rugu kutoka Karagwe mkoani Kagera wakishangilia na
kitita cha Shilingi 600,000/=mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za
mashindano ya Balimi Ngoma Mkoa wa Kagera yaliyofanyika katika Uwanja wa
Kaitaba Bukoba mjini.
Baadhi
ya washiriki na mashabiki wa Balimi Ngoma wakishuhudia fainali za mashindano ya
Ngoma mkoa wa Kagera yaliyofanyika
katika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mjini.
FAINALI za
mashindano ya Ngoma za Asili ngazi ya
mikoa zijulikanazo kama “Balimi Ngoma Festival 2014” Mkoani Kagera kikundi cha
Rugu chenye makazi yake Karagwe kimefanikiwa kuwaa ubingwa wa Mkoa wa
Kagera na kuzawadiwa fedha taslimu
Shingi 600,00/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa Kagera katika fainali
za Kanda zinazotarajiwa kufanyika Augusti 16,2014 Mkoani Mwanza.
Nafasi ya
pili ya mashindano hayo ilichukuliwa na Kikundi cha Rugoloile cha mjini Bukoba
ambacho kilizawadiwa fedha taslimu Shilingi 500,000/= pamoja na tiketi ya
kuwakilisha Mkoa katika fainali za Kanda.
Nafasi ya
tatu ilichukuliwa na kikundi cha Abagambakamo cha Muleba ambacho kilizawadiwa fedha taslimu Shilingi
400,000/= na nafasi ya nneilichukuliwa na kikundi cha Alute Continue ambacho
kilizawadiwa fedha taslimu shilingi 300,000/=.
Nafasi ya
tano mpaka ya mkumi ilichukuliwa na Uviti Ruzinga,Chupukizi,Kasharu,Kabete cha
Ihangilo,Jipe Moyo na Upendo Musira hivi vilizawadiwa kifuta jasho cha
150,000/= kila kikundi.Jumla ya Vikundi 11 vilijitokeza kushiriki fainali hizo
za Mkoa wa Kagera ngazi ya Mkoa kwa Mwaka 2014.
Akizungumza
na kwa nyakati tofauti Meneja matukio wa Kanda ya Ziwa, Erick Mwayela alisema Sababu
msinigi ya kuwepo kwa Mashindano ya Balimi Ngoma za Asili ni kuenzi na kulinda
utamaduni wa Kitanzania.
Mwayela aliongeza pia kuwa wao Kampuni ya Bia nchini ni
sehemu yao ya kurudisha fadhila kwa watumiaji wa Kinywaji cha Balimi Extra
Lager pamoja na vinywaji vyote vya Kampuni ya Bia Tanzania(TBL).
Fainali za Mkoa wa Kagera zilifanyika katika Uwanja wa
Mkoa wa Kaitaba na fainali za Kanda za mashindano ya Balimi Ngoma zinatarajiwa
kufanyika August 16,2014 jijini Mwanza kwa kushilikisha vikundi viwili viwili
kutoka Tabora, Shinyanga, Bukoba, Musoma
na Wenyeji wa mashindano Mwanza.
No comments:
Post a Comment